Mahakama
nchini Burundi imemwachilia kwa dhamana kiongozi mmoja mkuu wa upinzani
aliyekabiliwa na kashfa za ngono pamoja na ulaji rushwa.
Wafuasi
wake wanasema kuwa mashitaka hayo yalikuwa njama ya serikali kumzuia
kushiriki uchaguzi mkuu kugombea urais dhidi ya Rais wa sasa Pierre
Nkurunziza.
Frederic
Bamvuginyumvira, makamu wa zamani wa Rais na kiongozi wa chama cha
Front for Democracy (frodebu), alikamatwa mwezi Disemba akiwa ''katika
kitendo cha ngono katika danguro,'' alisema afisaa mmoja wa mahakama.
Bwana
Bamvuginyumvira alinyimwa dhamana mwezi Disemba lakini hapo jana
mahakama ikatoa amri hiyo kutokana na hali yake mbaya ya kiafya.
Mahakama ilisema kuwa anaweza kuachiliwa aweze kupata matibabu ya shinikizo la damu.
Wakili
wake Fabien Segatwa, alisema kuwa ''mahakama ya kupambana na ufisadi,
imeamuru aachiliwe kwa dhamana na dola 600. Bwana Bamvuginyumvira hana
sababu ya kuwa mahakamani kwani hana makosa yoyote. ''
Bamvuginyumvira,
kiongozi anayeheshimika sana nchini Burundi, alisifika sana kwa kuwa
mkali katika kupambana na rushwa na alikuwa makamu wa Rais kati ya mwaka
1998 hadi 2001. Kadhalika anaonekama kama mwanasiasa mwenye uwezo wa
kumenyana na Rais katika uchaguzi mkuu.
Wengi wanaona kama huenda akajitosa kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015.
MJUMBE sr
Post a Comment