Unknown Unknown Author
Title: SHANGAZI WA RAIS OBAMA AFARIKI DUNIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Shangazi wa rais Obama Zeituni Onyango ambaye kwa wakati fulani alinyimwa hifadhi  Marekani lakini akaendelea ku...
9E7F28FD-C45A-4887-A253-1FC94FFC74B1 w640 r1 s 4e544

Shangazi wa rais Obama Zeituni Onyango ambaye kwa wakati fulani alinyimwa hifadhi  Marekani lakini akaendelea kuishi kinyume cha sheria kwa miaka kadhaa katika jimbo la Masachussets amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61.
Wakili wa masuala ya Uhamiaji wa Onyango amesema amefariki katika hospitali moja baada ya kuugua ugonjwa saratani na matatizo ya kupumua . Aliugua tangu mwezi January.
Onyango alihamia Marekani kutoka Kenya mwaka 2000 na alinyimwa hifadhi ya kisiasa na jaji wa Uhamiaji mwaka 2004. Hakuondoka nchini na aliendelea kuishi kwenye nyumba za umma huko Boston. Hali yake ya ukaazi wa Marekani ilitangazwa hadharani siku chache kabla ya Bw.Obama kuchaguliwa rais Novemba 2008. 
chanzo:VOA

MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top