Unknown Unknown Author
Title: UKAWA WASAINI HATI YA USHIRIKIANO KATIKA CHAGUZI MBALIMBALI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Vyama vinne vya siasa vya upinzani vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi-UKAWA- vimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano ya kufanya k...

Vyama vinne vya siasa vya upinzani vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi-UKAWA- vimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano ya kufanya kazi pamoja katika chaguzi mbalimbali ikiwemo uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge unaotarajiwa kufanyika mapema mwakani.

Akisoma makubaliano hayo kwa niaba ya makatibu wa kuu wa vyama hivyo, katibu mkuu wa Chadema Dokta Wilbrod Slaa amesema chini ya makubaliano hayo vyama hicho vimekubaliana kuuwisha sera za vyama hivyo kwa kuchukua yale yanayofanana ili kuwa na kauli zinazofanana wanapozungumza na wananchi, pamoja na kushirikiana katika mchakato wa kuelimisha wananchi kupiga kura ya hapa kwa katiba mpya inayopendekezwa. 
 
Wakizungumza baada ya kusaini hati ya makubaliano, mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema amewatoa wito kwa viongzoi wa chama hicho katika mikoa kutokwamisha mipango ya Ukawa kwa kuwa ni mpango wa mungu na kuwataka vingozi wa vyama vinavyounda umoja huo kuhacha kukaa maofisi kwenda kwa wananchi kuendeleza mapambano, huku mwenyekiti wa CUF taifa Prof Ibrahimu Lipumba amewataka wananchi kutopiga kura ya ndiyo kwa katiba inayopendekezwa ili kuwezesha rasimali za nchi zitumike kwa faida ya wananchi wote. 
 
Aidha kwa upende wao mwenyekiti wa chama cha NCCR- Mageuzi mhandisi James Mbatia amewataka viongozi wa vyama hivyo katika mikoa kukaa kungalia wagombea wanaokubalika bila ya kujali chama na kuhacha kulalamika ili kuwasaidia watanzania kupata maendeleo kupitia rasilimali zao, huku mwenyekiti wa chama cha NLD Dkt Emmanule Makaidi akisisitiza umuhimu wa kujenga umoja utakaosadia kuleta mageuzi yatakayoleta mchango mkubwa kiuchumi. 
 
Makubaliano yamefanyika katika viwanja vya Jangwani jiji Dar es Salaam na kushuhudiwa na maelfu ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa vyama hivyo walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali ambao wengie wao wameingia kwa maandamano kutoka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
 

LIKE Ukurasa wetu MJUMBE BLOG facebook au Tutembelee Mtandaoni kwa kuandika MJUMBE BLOG Upate picha,Matangazo,Habari Muhimu na Taarifa Mpya kila Mara

@Mjumbe Blog Volunt

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top