Naibu katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba amewataka wajumbe wa Bunge maalumu la katiba wanaotaka nyongeza ya posho kujiondoa katika bunge hilo kama hawaridhiki nayo...
Akizindua kampeni za uchaguzi za uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kalenga kwa kumnadi mgombea ubunge wa Chama hicho Godfrey Mgimwa.Nchemba;Serikali haiwatendei haki Watanzania kama itakubaliana na matakwa ya baadhi ya wabunge wanaojali matumbo yao kwa kutaka nyongeza ya posho..!
Nchemba alisema posho wanayopewa wabunge hao imezingatia hali halisi ya nchi na kwamba hatakubali iongezwe..Anasema badala ya kudai nyongeza ya posho,Wabunge wanaoshiriki bunge hilo wanatakiwa waonyeshe uzalendo na kutumia fursa hiyo muhimu ili wawawakilishe Watanzania wenzao kutengeneza sheria mama ya nchi.
Na Mjumbe Jr
Mbozi.
Post a Comment