Mahakama ya kimataifa ya jinai
ICC imempata na hatia ya uhalifu wa kivita mbabe wa kivita kutoka
Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Germain Katanga.
Hata hivyo Katanga hakukutwa na hatia katika shtaka la udhalilishaji wa kijinsia.Katanga ni mtu wa pili kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC tangu ianzishwe mjini The Hague, Uholanzi mwaka 2002.
Katika shambulio hilo lililotokea mnamo Februari 24, 2003 watu 200 waliuawa katika kijiji cha Bogoro karibu na mpaka wa Uganda,Katanga wakati huo akiwa Kamanda wa kundi la waasi la Patriotic Resistance Force of Ituri (FRPI) lililotekeleza mauahi hayo.
Germain Katanga kwa jina la utani Simba alikanusha mashtaka hayo yote dhidi yake .
Chanzo:BBC SWAHILI
Na Mjumbe Jr
Mbeya
Post a Comment