Rais Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete (mwenye koti jeusi katikati) akiwa na baadhi ya
Mawaziri, Wabunge na Viongozi wa mkoa wa Tanga wakishiriki kuifungua
rasmi barabara ya Handeni – Mkata na Handeni - Korogwe huko mkoani
Tanga.
Rais Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete (aliyenyoosha mkono) akifurahia jambo na Waziri
wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anayempongeza kiongozi wa
kikundi cha ngoma ya Selo baada ya kutumbuiza wakati wa sherehe za
ufunguzi wa barabara ya Mkata – Handeni - Korogwe. Anayeangalia (kulia)
ni Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Handeni Dkt. Abdallah
Kigoda.
Rais Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya
Mawaziri, Wabunge na Viongozi wa mkoa wa Tanga wakishiriki kukata utepe
kuifungua rasmi barabara ya Handeni – Mkata na Handeni - Korogwe huko
mkoani Tanga.
Sehemu ya barabara ya Handeni – Mkata.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amewataka wakazi wa Handeni na maeneo inakopita barabara ya Mkata –
Handeni na Korogwe – Handeni kutumia ipasavyo fursa ya kupatikana kwa
barabara hizo za lami kuyaboresha maisha yao.
Rais
Kikwete alitoa rai hiyo wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara
inayoinganisha Makao Makuu ya Wilaya ya Handeni na barabara kuu ya Tanga
- Dar es Salaam kupitia Mkata na upande mwingine kuunganisha na
barabara kuu ya Tanga – Moshi – Arusha kwa upande wa Korogwe.
Mhe. Rais
ameelezea kuwa lengo la Serikali ni kuona kwamba, barabara ya Mkata
hadi Handeni inaendelezwa hadi Kondoa kupitia Kiberashi kwani kufunguka
kwa ukanda huu kutakuwa ni chachu kubwa ya kuinua shughuli nyingi za
kiuchumi hasa kwa sekta ya kilimo katika maeneo hayo inakopita barabara
hiyo.
Akiwasilisha
tarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara
Tanzania (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale alielezea kuwa barabara ya
Mkata - Handeni ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ina urefu wa
kilometa 53.2 ikiwa imejengwa na MkandarasiSinohydro Corporation Ltd
kutoka Jamhuri ya Watu wa China kwa gharama ya Shilingi bilioni 57.3.
Eng. Mfugale alibainisha kuwa mkataba wa mradi huu ulisainiwa mwezi June
2009 na kazi zikakammilika mwezi Novemba 2012 baada kutatua changamoto
ambazo zilikuwa zinakwamisha kukamilika kwa muradi huo mapema zaidi kama
ilivyokuwa imepangwa kimkataba.
Ufunguzi
wa barabara hiyo umeenda sambamba na ufunguzi wa barabara ya Korogwe
hadi Handeni ambayo vile vile imekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Akitoa
tarifa kuhusu miradi huo wa Korogwe – Handeni, Mtendaji Mkuu wa TANROADS
Eng. Patrick Mfugale alielezea kuwa MkandarasiSinohydro Corporation Ltd
ndiye pia iliyeijenga barabara hiyo ambayo ina urefu wa kilometa 65.
Mkataba wa Mradi huu ulisainiwa mwezi June 2009 na kazi zikakamilika
mwezi June 2013 na imejengwa kwa ghrama ya Shilingi bilioni 63.2. Kiasi
cha Shilingi bilioni 3.3 kimelipwa kama fidia kwa wale waliofuatwa na
barabara hiyo katika baadhi ya maeneo.
Naye
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akielezea baadhi ya faida
zitakazopatikana kutokana na kujengwa kwa barabara hizo alibainisha
kuwa barabara ya kutokea Korogwe hadi Handeni ndiyo barabara
itakayosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa magari katika
barabara kuu ya TANZAM hasa kwa wasafiri na wasafirishaji wanaotokea
maeneo ya Iringa, Mikumi na mengineyo katika ukanda huo.
Waziri
Magufuli alifafanua kwa kwa kupitia Mikumi, Kilosa, Turiani, Mziha hadi
Handeni na kuelekea Korogwe au Mkata mkoani Tanga kunapunguza zaidi ya
kilometa 120 tofauti na kuzungukia Morogoro na Chalenze.
"Hivi
sasa mtu anayetokea Iringa analazimika kupitia Mikumi na Morogoro mjini
hadi Chalinze ndipo aelekee Tanga, mzunguko ambao ni mrefu kulinganisha
na barabara hii ya kupitia Mikumi, Kilosa Magole, Mziha hadi Handeni"
alisistiza Waziri Magufuli.
Kwa
upande mwingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete aliwafahamisha wananchi waliohudhuria kwa wingi
katika sherehe hizo kuwa, tayari upembuzi yakinifu na usanifu wa kina
umekamilika kwa barabara inayoanzia Handeni kuelekea Kiberashi hadi
Kwamtoro mkoani Dodoma.
Rais
Kiwete aliabinisha kuwa hatua hiyo pia imefikiwa kwa barabara ya
Handeni, Mziha, Dumila, Kilosa hadi Mikumi. "Hatua inayofuata ni
kutafuta fedha za kujenga maeneo katika sehemu hizo ambayo bado
hayajapata makandarasi" alifafanua zaidi Rais Kikwete.
Hata
hivyo Mhe. Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaasa wasafirishaji kuzingatia
masuala ya usalama barabarani kwa kupakia mizigo kulingana na viwango
vilivyowekwa kisheria. Alielezea kuwa moja ya adui wakuu waharibifu wa
barabara ni uzidishaji wa mizigo kupita viwango vilivyowekwa kisheria.
Mheshimiwa
Kikwete anaendelea na ziara yake mkoani Tanga ambapo pia ataweka jiwela
msingi kuzindua ujenzi wa barabara ya Korogwe – Mkumbara.
chanzo:PT
MJUMBE Sr
Post a Comment