Unknown Unknown Author
Title: URUSI YATENGWA KATIKA KUNDI LA G7
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Viongozi wa kundi la mataifa saba tajiri zaidi duniani, G-7, wanafanya mazungumzo kwa siku ya pil...
wamejitolea_67383.jpg
Viongozi wa kundi la mataifa saba tajiri zaidi duniani, G-7, wanafanya mazungumzo kwa siku ya pili mfululizo hivi leo mjini Hague, Uholanzi ajenda kuu ikiwa ni hatua ya Urusi kunyakua jimbo la Crimea kutoka Urusi.
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998, Moscow imenyimwa kiti katika kongamano hilo. Mkutano wa dharura wa G-7 uikubaliana kufutilia mbali kundi la G-8, kundi la mataifa manane tajiri zaidi duniani, ambalo linaishirikisha Urusi.
Viongozi wa mataifa ya kundi hilo wameonya kuwa vikwazo zaidi vitatolewa iwapo Urusi itaingia maeneo ya mashariki au Kusini mwa Ukraine ikiwepo kulenga sekta ya kawi nchini Urusi. Lakini Marekani kadhalika imesisitiza kuwa fursa ya kusuluhisha mzozo huo wa njia ya kidiplomasia ingalipo.
Chanzo:PT

MJUMBE Sr




About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top