Unknown Unknown Author
Title: JESHI LA POLISI LAZUIA MKUTANO WA UKAWA,ZANZIBAR
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
               Picha ya Maktaba yetu POLISI YAZUIA MKUTANO WA UKAWA ZANZIBAR Jeshi la Polisi Zanzibar limeendelea kuuchelewesha...
               Picha ya Maktaba yetu

POLISI YAZUIA MKUTANO WA UKAWA ZANZIBAR
Jeshi la Polisi Zanzibar limeendelea kuuchelewesha mkutano wa wanachama wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kwa madai kwamba hakuna askari wa kutosha kuulinda. Ukawa ni muungano wa vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, DP na wajumbe 25 kutoka kundi la wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete.
Awali, mkutano huo ulipangwa kufanyika Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Kibandamaiti, Unguja lakini jeshi hilo liliuzuia kwa madai ya kuwapo kwa habari za kiintelijensia dhidi ya tishio la maisha ya watu.
Hata hivyo, Msemaji wa Polisi Zanzibar, Mohamed Mhina alisema umezuiwa kwa sababu askari na maofisa wa polisi wanaotakiwa kuusimamia wako Dar es Salaam katika maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hivyo mkutano huo hautafanyika hadi Aprili 30, mwaka huu.
“Tumekutana nao (CUF walioomba kibali kwa niaba ya UKWAW) na kukubaliana kwamba mkutano huo ufanyike Aprili 30 kwani askari waliopo hivi sasa ni wachache hawawezi kutosha kusimamia ulinzi kutokana na aina ya mkutano wenyewe. Hata hiyo siku hiyo hakutakuwapo na maandamano, bali wataruhusiwa kufanya mkutano pekee na siyo vinginevyo.”
Katibu wa UKAWA nje, Shaweji Mketo alisema wamekubaliana na jeshi hilo la Polisi kwamba Aprili 30 tutafanya mkutano pale Kibandamaiti na siku inayofuata tutafanya mkutano Pemba.

MJUMBE Sr
Like · · · 118

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top