Unknown Unknown Author
Title: KIJIJI CHENYE KUSAWILI UJAMAA NA SOGEA YA ENZI ZA MWALIMU:KIJIJINI AMANI HAPA MAJI YABOMBA KILA BAADA YA MTAA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
    Picha Kijijini,Amani;Ludewa Bomba la Maji Likiendelea Kutiririsha Maji baada ya Kufunguliwa na Mdau wa Mjumbe  Blog.    Pichani Md...
    Picha Kijijini,Amani;Ludewa
Bomba la Maji Likiendelea Kutiririsha Maji baada ya Kufunguliwa na Mdau wa Mjumbe  Blog.
   Pichani Mdau Akitaka Kuhakiki Mwenyewe!
   Pichani Mabinti hawanao Kamera Yetu iliwanasa wakifaidi Maji ya Kijijini Amani,Ludewa

Kihistoria Kijiji cha Amani,Kilichopo kata ya Mundindi Tarafa ya Liganga Wilaya ya Ludewa ni Matokeo ya ile Kampeni ya SOGEA ili kujenga vijiji vya UJAMAA! Kwa Wana Historia watakuwa wamesha Elewa Kijiji hiki kilianza kujengwa Rasmi lini.Maelezo ya SOGEA na UJAMAA yanajitoshereza kubashiri Mwaka.



 Kijijini Amani,Madukani ama kijiweni kama wanavyo paita wakazi wake

Wakazi wa Kijiji Hiki wana jishughulisha zaidi na Kilimo cha Mahindi kama zao kuu na Mazao mengine yanazalishwa japo si kwa wingi ikilinganishwa na Mahindi ambayo wana kijiji wame yageuza kuwa kama Zao la Biashara.
Pia Kijiji kina Utajiri wa Misitu na Mabonde yenye Rutuba na Maji yanayo dumu kwa Msimu mzima wa Mwaka,kuna miti ya Asili na Miti ya Kupandwa.
Kijiji kime kuwa miongoni mwa vijiji vya Wilaya ya Ludewa vyenye Rasilimali mbali mbali,yakiwemo Madini kama Chuma,Dhahabu na Mengine Utafsiti Unaendelea Kufanyika.Wananchi wengi kijijini hapo ni wafugaji wa Ng'ombe ambao ndio nyenzo kuu ya Kilimo na Kipato kwa wengine kuuzwa ndani ya kijiji na nje ya kijiji.
Kijiji cha Amani,ni miongoni mwa Vijiji vichache nchini vinavyo toa Taswira halisi ya Historia ya nchi yetu hasa enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,ambaye alihamasisha na Hata kuhimiza watu Wajikusanye Sehemu moja ili kuwafikishia huduma za Kijamii kwa Ufanisi na Urahisi zaidi,Ukifika Kijijini hapo pia Utakutana na tunu hiyo ambayo kwa sasa ni adhimu mno kuipata nchi mwetu.Wakazi wengi Wanao ishi Kijijini Amani wana Udugu wa Damu na hata wa kuoleana kwa kiasi kidogo sana kuna wageni wanaishi kijijini,Amani ambao wengi wao ni Wafanya Kazi wa Kiserikari na Msimu wa Mavuno Kuna Muingiliano mkubwa kijijini kutokana na Mbiashara kushamiri huingiza wageni pia.
 Baadhi ya Mifugo iliyopo Kijijini Amani,kama inavyo onekana Pichani

Mwakajana Baadhi ya wanakijiji walifanikiwa kusambaza Umeme wa Maji ndani ya kijiji kwa baadhi ya Wakazi wa kijiji hicho na bado Kuna wanao fanya Kila Wawezalo ili kuweza kuleta umeme wa Uhakika zaidi kwa matumizi ya Kijiji kizima,tofauti na Awali Umeme uliokuwa ukitumiwa na baadhi ya wakazi ulikuwa Umeme wa Mionzi ya Jua tu.
Mimi niki kitazama kijiji cha Amani nina Iona Historia ya Taifa Yangu Dhahiri!
   Mto Ukiwa Umechepushwa ili Kuvuna Maji ya Kufulia Umeme
Picha Tatu Zikonesha Jinsi Umeme Ulivyo Zalishwa Kutokana na Maporomoko ya MAJI!

Kinacho kifanya kijiji  hiki kamera yetu ikipe Umakini wa kipekee ni Pamoja na kuwa Mbali sana kutoka makao makuu ya Wilaya ya Ludewa(Ni zaidi ya 150,kufika Makao makuu) na Zaidi ya 135 Km Kufikia Barabara kuu ya Njommbe-Songea Lakini Kina Mahitaji ya Msingi kwa Binadamu yote na kinajengwa katika misingi endelevu zaidi kila siku.Sio vile vijiji vya msimu wa Kiangazi bali Hata Masika maisha yanaendelea.Haya ni matokeo Chanya ya Dhana ya SOGEA na Ujamaa,nchini mwetu enzi za Mwalimu.
   Nguvu ya jua ndio Chimbuko pia!

Hapo ndipo Kambi la MJUMBE Sr anapo kuwa yupo Ludewa,Njombe;Maana Wadau hawa kawii kuniimbia ule Wimbo wa "YAHAYA Unaishi Wapiiiii....".

Karibuni Ludewa,Karibuni Kijijini Amani!
Picha Zote Kwa Hisani ya Kamera yetu/Maktaba Yetu

Elasto Mbella
Mbeya
0752025002

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top