Unknown Unknown Author
Title: MUUNGANO WETU UDUMU LAKINI TUNAIOMBA TANGANYIKA HURU!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
    "UNATAKA KUSIKILIZA LIPI;NIKWAMBIE UKWELI au UNATAMANI NIKUDANGANYE?" Hayo Maneno yapo Kwenye Moja ya Mahojiano ya Ali...
 
 
"UNATAKA KUSIKILIZA LIPI;NIKWAMBIE UKWELI au UNATAMANI NIKUDANGANYE?" Hayo Maneno yapo Kwenye Moja ya Mahojiano ya Aliye wahi kuwa Mwigizaji maarufu nchini Marehemu Steven Kanumba(RIP).Kweli kuna kipindi Kabla hauja amua kumweleza mtu jambo analo taka kujua kutoka kwako Lazima Umusome kwanza yeye anataka nini? Na ikibidi umuulize... Anataka Kusikiliza Uongo au Ukweli? Marafiki Zangu walio wengi wanapenda kusikiliza Uongo ukiwadanganya ndio watakupenda zaidi.Leo ni Miaka 50 Tangu Wazanzibar Waungane na Tanganyika na hata kuzaliwa nchi moja inayo itwa TANZANIA,Nchi ambayo wengi ndiyo imetulea.Kume kuwa na mvutano wa Muundo wa Serikari katika Bunge Maalumu la katiba wa ama kufuata Maoni ya wananchi(Haya yamepewa jina ni Maoni ya wachache au Maoni ya Warioba) yanayo pendekeza muundo wa Serikari Tatu na Maoni ya Wajumbe Walio Wengi ndani ya Bunge la katiba Msimamo wao Ukisimamiwa Rais wa nchi pia! wao wana sisitiza kuwa pamoja na Changamoto zinazo zikabili Serikari mbili,lakini zina weza kutatulika na kuzungumzika,hivyo hakuna umuhimu wa kuongeza mzigo zaidi wa Serikari ya tatu.Nahapa kwa Utashi wangu hawa wanao ogopa mabadiliko(Wahafidhina) wana kuja na hoja za kutishia wananchi kuwa kama Serikari zikiwa Tatu iyo ya tatu itakosa nguvu na hata inaweza kupelekea jeshi kuasi na kushika hatamu kwa siku zijazo! Hapa ndipo wengi wame ibuka kuanza kumshambulia Mzee Jaji Joseph Warioba na kusema Alianzaje kukubali haya maoni ya muundo wa Serikari tatu? Hapa Maoni ya wana nchi yamegeuzwa jina na yana itwa maoni ya Warioba! Kun a uvumi wa Vitisho vingi kwa raia kuhusu muundo wa Serikari tatu kuliko hoja za msingi zilizo tolewa na tume.Na hii katika ile Elimu ya Mantiki wataalamu wana ita "ad hominem" yaani badala ya mtu kujibu hoja za Mhusika wana anza kumushambulia na hata ikibidi kumubatiza majina mabaya.Wajumbe wengi na rais wa jamuhuri ya muungano wao wana hitimisha kwa kupigia chapuo muundo wa serikari Mbili tu,katika hili wao wana sisitiza kuwa ni ama serikali mbili au kama hamtaki tuikabidhi nchi jeshi! Hili nalo katika Elimu ya mantiki wataalamu wanalifafanua kama "a fallacy of two dilema" yaani baada ya wewe kutoa hoja,anaye ijibu hoja yako ana kupa jibu kwa machaguo mawili pekee hapa ndio kuna msemo ule wa Ukitaka usuke au unyoe! Lakini Ukijiuliza hivi kuna mitindo miwili tu ya usukuaji nywele? Hakuna Afro,Hakuna Rasta? hakuna Viduku na mitindo mingine? Hapo ndipo tuna sema hoja si kuchagulia muhusika majibu unayo tamani kuyasikiliza wewe,Mwache aje na Majibu yake na msimamo wake huenda hata wewe kuna jambo utajifunza.Kuna wanao tetea muundo wa Serikari mbili kwa kuhusianisha na Umri wa wengi walio zaliwa baada ya muungano na kuhitimisha kirahisi kuwa kwasababu Umri wa Muundo wa serikari mbili ni mkubwa kuliko hao wachache wanao dai muundo wa Serikari tatu basi waulinde muundo ulio walea;Hii hoja nayo haina mashiko kwani,Sisi(Binadamu) ndio tulio chagua muundo wa serikari amabayo kwa Muda na wakati wake Tuliamini inatufaa na Sio muundo wa Serikari ulio tuchagua sisi! yaani Hakikuundwa kijiko ndio vikaumbwa vidole bali viliumbwa Vidole ndio kikaundwa kijiko! Katika Hili la Kaluli yangu kuhusu muundo wa Serikari ninayo itamani iwepo;lisi Husianshwe na Imani yangu,Itikadi yoyote ile wala Shughuli yngu yoyote ile niifanyayo.Huo ni Mtazamo wangu na huo ndio ukweli wa Ninacho Kitamani mimi,Vinginevyo Nitakuwa nimekudanganya.
SERIKARI TATU NDIO MUUNDO PEKEE Utakao Kidhi mahitaji ya Muda na Wakati Tulio nao.
Elasto Mbella
MBEYA

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top