Unknown Unknown Author
Title: NACTE YATOA UTARATIBU MPYA KUOMBA VYUONI KWA 2015!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limesema kuanzia mwaka huu wa masomo, wanafunzi wanaotaka kujiunga na masomo ngazi ya as...



Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limesema kuanzia mwaka huu wa masomo, wanafunzi wanaotaka kujiunga na masomo ngazi ya astashahada na stashahada ya utabibu na ualimu, watatakiwa kuomba katika mfumo wa pamoja wa mtandao wa Central Admission System (CAS) na siyo vyuoni kama ilivyozoeleka.

Katibu Mtendaji wa NACTE, Dk. Primus Nkwera, alitoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maazimio mbalimbali ya kikao cha 56 cha baraza hilo.

Alisema miaka ya nyuma wanafunzi wa utabibu na ualimu waliotaka kujiendeleza kimasomo, waliomba moja kwa moja vyuoni hali ambayo ilisababisha kuwapo kwa mgongano wa wanafunzi na huku baadhi vikidahili wasio na sifa.

“Mfumo huo utatuwezesha siku ya mwisho ya kuomba waweze kutoa majina waliochaguliwa ili kusiwe na mwingiliano na zoezi hilo litafanywa na NACTE; tumefungua maombi hadi Julai 31, mwaka huu,” alifafanua.

Alisema udahili wa wanafunzi kwa ngazi ya astashahada, stashahada na shahada, umeanza Baraza limetoa usajili wa muda mfupi na mrefu kwa vyuo mbalimbali 17; ambapo usajili wa kudumu umetolewa kwenye vyuo sita huku usajili wa wa miaka mitano kituo kina uwezo wa kuendesha mafunzo.
 
MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top