Unknown Unknown Author
Title: PAPA WAWILI WATANGAZWA WATAKATIFU!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Umati mkubwa wa watu wamekusanyika mjini Vatican kushuhudia tukio...
Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani
Umati mkubwa wa watu wamekusanyika mjini Vatican kushuhudia tukio la kihistoria ambapo viongozi wawili wa zamani wa Kanisa Katoliki, Papa John Paul II na Papa John XXIII wametangazwa watakatifu.
Ibada iliyoendeshwa kwa pamoja kati ya Papa Francis na mtangulizi wake Papa Benedict XVI imeangaliwa na karibu mahujaji milioni moja na wengine mamilioni ya watu kupitia matangazo ya televisheni na redio.
Karibu ujumbe wa wageni 100 wamehudhuria sherehe hiyo, wakiwemo kutoka koo za kifalme na wakuu wa nchi na serikali.
Hii ni mara ya kwanza kwa papa wawili kutangazwa kwa wakati mmoja kuwa watakatifu.
Waandishi wa habari wanasema hatua hii inachukuliwa kama njia ya kuziunganisha kambi mbili za wapenda mageuzi na wasiotaka mabadiliko ya sheria katika Kanisa Katoliki.
MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top