Unknown Unknown Author
Title: PITIA HAPA UYAJUE MABADILIKO YA NJIA ZA KUINGIA NA KUTOKA DALADALA POSTA JIJINI DAR KUANZIA LEO 28 APRIL 2014!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
 Viongozi wakijadiliana wakati wa zoezi la kuweka Alama muhimu za barabarani Katikati ya Jiji tayari kwa mabadikiko ya mielekeo ya b...

 Viongozi wakijadiliana wakati wa zoezi la kuweka Alama muhimu za barabarani Katikati ya Jiji tayari kwa mabadikiko ya mielekeo ya barabara za Samora na Sokoine unaoanza Jumatatu 28/04/2014. 
 Vijana wakiweka kibao cha alama barabarani.
Jana Aprili 26, 2014 zoezi la kuweka Alama muhimu Katikati ya Jiji la Dar es Salaam limekamilika tayari kwa mabadikiko ya mielekeo ya barabara za Samora na Sokoine unaoanza Jumatatu 28/04/2014. Kwa daladala itakuwa kama ifuatavyo:

Habari na Picha na Deo Mutta, DART

1. Daladala Zote zinazotokea Barabara ya Ally Hassan Mwinyi zitaingia mjini kupitia Bibi Titi na kukata kushoto kuingia barabara ya Makataba na kuishia Posta Mpya na kutoka kwa kuzunguuka Mnara wa Askari na kushuka na Maktaba na Kupinda kulia kuingia Bibi Titi na baadaye All Hassan Mwinyi.

2. Daladala Zote zinazotokea Barabara ya Morogoro zitapinda kushoto kuingia Bibi Titi na Kupinda kulia kuingia Maktaba hadi Posta Mpya. Zitatoka kwa kuzunguuka Mnara wa Askari na kuingia Samora hadi Clock Tower na kuingia Uhuru na Kupinda kulia kuingia Bibi Titi na Kupinda kushoto kuingia Morogoro.

3. Daladala zinazotokea Barabara ya Uhuru zitakwenda moja kwa moja hadi Clock Tower na kuingia Barabara ya Railway na Kupinda kushoto kuingia Sokoine na kuishia Stesheni. Zitatoka kwa kupitia Samora kutokea station na kuingia Uhuru kupitia mnazi mmoja.

4. Daladala zinazotokea Barabara ya Nyerere zitapita bibi Titi na kukunja kulia kuingia Uhuru hadi Clock Tower na kuingia Railway na kukunja kushoto kuingia Sokoine na kuishia Stesheni. Zitatoka kupitia Samora hadi Clock Tower na kuingia Nkurumah na kuingia Nyerere eneo la Cocabs.

5. Daladala zinazotokea barabara ya Kilwa Zitapitia Sokoine na kuishia Stesheni na kutoka kupitia Railway na kuingia Sokoine kuelekea Water Front.

Ufafanuzi Zaidi!

MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA TAREHE 28/04/2014. TRAFFIC CIRCULATION AT CBD

1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari (Askari Monument) hadi Clock Tower Magari kutakuwa na mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock Tower badala ya Askari Monument. 

2. Barabara ya Sokoine kuanzia Station hadi Makutano ya Mtaa wa Maktaba Posta Ya Zamani Magari yatakuwa yanaelekea Uelekeo mmoja wa Station Posta ya Zamani tofauti na ilivyo sasa Posta ya Zamani kwenda Station. 

3. Barabara ya Kivukoni Kuanzia Posta ya Zamani hadi Ferry itakuwa barabara ya mielekeo miwili (Two Ways).

4. Barabara ya Samora kuanzia Mnara wa Askari hadi Ocean Road Hospitali itakuwa ni barabara ya mielekeo miwili.

5. Daladala Zote zitakazotokea barabara za Makataba zitakunja kulia pembeni ya Jengo la NBC na hadi Makutano ya Mkwepu na kukunja kushito kuingia Sokoine pale Posta ya Zamani na baadaye kukunja kushoto kuingia Makataba na kurudi Posta Mpya .

Key:
1. RANGI YA NJANO - Njia ya Uelekeo Mmoja {One Way}.

2. RANGI YA BLUE MPAUKO - Njia ya Mielekeo Miwili {Two Way}

3. RANGI YA KIJANI - Mitaa ya Kutembea kwa Miguu Magari marufuku {Walking Streets}

4. RANGI NYEKUNDU - Barabara za kupita Daladala

5. RANGI YA BLUU ILIYOIVA - Barabara za DART

6. DUARA ZA NJANO - Mzunguuko {Roundabout}

7. MSALABA WA KIJANI - Makutano yenye Taa za kuongozea Magari {Singnalized Intersection}

Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Ofisi za DART
UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA.

AU.
OFISI YA MHANDISI WA MANISPAA YA ILALA
 
MJUMBE sr


MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top