Wadau;
Wa Tanzania tuna hulka ya ajabu sana,tume kuwa wapigaji au Madilunga kila mahali! Ubunifu wetu mwingine huwa una washangaza hata wazungu;kwani hutufanya sio tu tuonekane watu wa ajabu bali hutuingiza moja kwa moja katika kundi la wanyama(Reptilia,Amfibia).
Chanzo chake ni ule utamaduni ulio jengeka wa kufikiri kwa kuisikiliza milio ya mingurumo ya matumbo yetu(short sighted-Myopia).Tume kuwa ni watu wenye maono ya reja reja,Tume kuwa kama mzazi anaye jifikiria yeye tu na kusahau hatima ya watoto wake mwenyewe;Anapanda mchicha na kuikata minazi yote.
Tofauti na wenzetu(wajomba zetu) ambao daima wamejijengea utamaduni wa kuvalisha viona mbali katika Utashi wao,Fikra zao,Weredi wao,Utashi wao na Katika Akili zao.Ili kufikia maono yao kama jamii na Taifa kwa ujumla.Wenzetu wamekuwa sio watu wa reja reja au Madilunga katika masuala yao ya Msingi.
Mr Ton Akiteta Jambo kwa Lugha ya kwao na Mwenzake Walio Ongozana Nae
Mfano;Ni Rahisi sana kwa wa Tanzania kuiba Nondo na saruji za kujengea Daraja la kijiji chao weneyewe,amablo watavuka wao na ndugu zao kesho na kesho kutwa kwa kupunguza uwiano sahihi wa vipimo na kutumia vipimo bandia na baada ya muda Mfupi daraja Daraja hubomoka na kuwa ua wao wenyewe na Jamaa zao na hapo ni kitambo kidogo tu baada ya kuzinduliwa kwa mbwembwe na viongozi waandamizi wa Kiserikari! Wajenzi wanajisahau wanapita palepale na kuutoa uhai wao.Na kwakuwa jamii yetu haina utamaduni wa kutafuta suluhu ya kudumu ya Matatizo yanayo jitokeza,Tukio hilo la Daraja kubomoka na kupoteza maisha ya raia wasio na hatia hupita na pengine huunganishwa na mapenzi ya MUNGU ili tu Kujustfy kitendo husika na Sio kuhusishwa na mapenzi ya wajenzi wa Daraja Bandia.Haya ndio matokeo ya kupoteza kumbukumbu ndani ya jamii.
Kutoka Kulia Mr Ton,Mtweve J,Vicent Mgina(Diwani),Mpiga Picha wa Mr Ton na Nyuma ya Kamera yetu Yupo Mjumbe Sr
Nina hakika ujio wa Mr Ton katika Tarafa ya Liganga kijijini Amani sio kuja kumtembelea Mtu flani,Ni ziara ya Kiutendaji zaidi.Nitashangaa sana kama Mr Ton atasema lengo lake kuu la kufika Tarafa ya Liganga ni kuja kuitazama Mbuzi wake aliye pewa zawadi na wana Liganga.Pili nitashangaa kam atasema amekuja kumusalimu kiongazi flani wa kijamii! Tatu nitashangaa sana kama Atasema lengo lake kuu lilikuwa kuja kuitembelea miradi ya watu binafsi,Hakika nitashangaa 'Kama nilivyo ushangaa Mwenge wa Uhuru'.
Nijuavyo mimi ujio wa Mr Ton kwa Mwamvuli wa SHIPO lengo lake kuu ni kutembelea miradi shirikishi kati ya jamii husika ya wana Liganga na watoa misaada na kuhakiki utumikaji wabmisaada hiyo,kwa kujionea mwenyewe.
Sijaona maelezo wala waraka usemao SHIPO tukisha maliza ujenzi wa Mabweni ya wasichana wazazi wata changia pango la vyumba ama pango la la nishati ya jua kwa ajili ya matyumizi ya mwanga kwa wanafunzi wakati wanajisomea.
Hayiyumukiniki wanao tamani kufanya Udilunga wa aina hiyo kwa mwamvuli wa ujio wa Mr Ton wapo kati yetu,wanatamani wapige Hela!
Kwakuwa Historia ipo,Baada ya Muda itawahukumu kwani Historia sahihi itahifadhiwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kabla sija hitimisha makala yangu nivema nika weka wazi maana ya msamiati "Dilunga" kama lilivyo tumika katika makala hii.Kwa Tafsiri isiyo rasmi "Dilunga" ni tapeli naye tumia lugha tamu tu ili kuwa laghai walengwa.Ma-Dilunga halisi huwa hawatumii bunduki,hawa tumii nguvu wala hawa mwagi damu ya watu ili kufanikisha lengo lao.Bali hupangila vema maneno,tungo na misamiati na kumteka mlengwa hata akajisikia yupo salama mikononi mwao;hushituka wakati tiari matapeli hao wame fanikisha Lengo lao kuu.Katika jamii usiombe ma dilunga wakapewa Ridhaa,wata waliza mpaka mkome.
Hitima;Niseme ujio wa SHIPO Liganga usigeuzwe Neema kwa Ma Dilunga.
(Makala ilichapwa Siku Chache Kabla ya Ujio wa Mr Tony/Karibu Tanzania Kutembelea Miradi ya SHIPO na Jamii Kijijini AMANI,LUDEWA tarehe 17 Februali 2014)
Elasto M Ngaya
NJOMBE/LUDEWA
0752025002
Post a Comment