Unknown Unknown Author
Title: UCHAFU WAHATARISHA AFYA ZA ABIRIA KITUO CHA MABASI UBUNGO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  BAADHI ya abiria wanaotumia Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT), wamesema afya zao ziko hatarini kwa kupatwa na magonjwa ya mlipuk...
http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/04/ubt_2.jpg 
BAADHI ya abiria wanaotumia Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT), wamesema afya zao ziko hatarini kwa kupatwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kusambaa kinyesi kituoni hapo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana, abiria hao walisema licha ya Halmashauri ya Jiji kukusanya ushuru kwa madai ya kukiweka kituo hicho katika hali ya mazingira ya usafi, hali ni tofauti.
Walisema kusambaa kwa kinyesi na harufu mbaya ilitokana na kufumuka chemba la majitaka kwa zaidi ya siku tano sasa, huku kukiwa hakuna juhudi zinazofanyika kuondoa kero hiyo.
John Charles, ambaye ni abiria, alisema alishangaa kuwaona watendaji wa jiji kufika katika eneo hilo huku wakishindwa kuchukua hatua za haraka kwa ajili ya kulinda afya za abiria.
“Hali ni mbaya, tumewaona watu wa jiji walikuja na kuangalia kisha wakaondoka bila kufanya 
chochote,” alisema.
Christina Donald, alishauri viongozi wanaohusika  kuangalia kituo hicho na kuchukua hatua za haraka ili kunusuru afya za abiria.
 Tanzania Daima 
 
MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top