Tangu
Ugonjwa Unaodhoofisha Kinga ya Mwili (Ukimwi) ulipogundulika mwaka
1983, zimekuwapo changamoto kuhusu maambukizi hayo. Kubwa ni maambukizi
ya mama kwenda kwa mtoto.
Kwa kawaida, maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) yanaweza kutokea kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Hali
hii inaweza kutokea kwa njia kuu tatu; wakati wa ujauzito, wakati wa
uchungu,wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua kwa njia ya
kunyonyesha.Kama hali hii isipodhibitiwa, uwezekano wa kutokea
maambukizi ni kati ya asilimia 20 mpaka 45. Kwa vigezo vyovyote vile
idadi hii ni kubwa na kazi ya Mpango wa Kitaifa Kudhibiti hali hiyo
(PMTCT) ni muhimu.
Asilimia
tano mpaka kumi ya maambukizi hutokea wakati wa ujauzito wenyewe,
asilimia kumi mpaka kumi na tano wakati wa uchungu na kujifungua na
asilimia tano mpaka ishirini wakati wa kunyonyesha.
Vipo vipengele mchanganyiko na hatarishi ambavyo kuwepo kwake kunaongeza uwezekano wa VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wake.
Wingi
wa virusi kwenye mwili wa mama, kiwango kidogo cha chembechembe za CD4
hali ambayo hutokea kwa wale wanaopata maambukizi kwa mara ya kwanza na
wale walio kwenye hatua za mwisho za maambukizi (AIDS) ni sababu
mojawapo.
Kiwango
cha maambukizi na ukali wake pia hutegemea na aina ya virusi. Uwezekano
wa maambukizi na kiwango chake viko juu zaidi kama mama ana virusi vya
HIV-1 kuliko aliye na aina ya HIV-2 .
Kwa bahati mbaya kirusi cha HVI-1 ndicho kinachopatikana zaidi Afrika.
Maambukizi
ya bacteria, malaria na magonjwa ya zinaa husababisha kondo la nyuma
kupitisha VVU kwa urahisi zaidi wakati wa ujauzito.
Kupasuka
kwa chupa zaidi ya saa nne wakati wa uchungu na kujifungua pia
huchangia maambukizi kutokea kwa kiwango kikubwa na hasa kama ana
maambukizi kwenye mfuko wa uzazi.
Vipengele
vingine hatarishi hutokana na wakati wa kunyonyesha kama magonjwa ya
kinywa kwa mtoto, matiti kuwa na vidonda au majipu, muda wa kunyonyesha
na kutumia chakula mchanganyiko na na maji kabla mtoto hajatimiza umri
wa miezi sita.
Mwananchi
MJUMBE Sr
Post a Comment