Unknown Unknown Author
Title: ADO SHAIBU:ATOA SHUKRANI KWA WATU WOTE WALIO HUDHURIA KWENYE MJADALA WA KITABU CHA "RUN FREE" CHA RICHADR MABALA! WAJUE BAADHI YA WASANII NA WATU MAARUFU WALIO HUDHURIA KWENYE MJADALA HUO!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SHUKRANI TOKA MOYONI Ukurasa wetu wa Kitabu Nilichosoma unatoa shukrani za dhati kwa watu wote waliohudhuria kwenye mjadala wetu wa kit...

SHUKRANI TOKA MOYONI
Ukurasa wetu wa Kitabu Nilichosoma unatoa shukrani za dhati kwa watu wote waliohudhuria kwenye mjadala wetu wa kitabu cha ‘Run Free’ cha Richard Mabala uliofanyika Jumamosi ya tarehe 17/5/2014 viunga vya Soma Book Cafe.
Mosi, shukrani za dhati ziwafikie Masoud Kipanya, Richard Mabala na Mama Elieshi Lema, waliokuwa wawasilisha mada wetu. Kama inavyofahamika, hawa wote ni watu wenye majukumu mengi na hivyo basi kukubali kwao kuhudhuria kwenye mjadala kumetupa moyo sana.
Kwa Masoud na Mabala, shukrani za ziada ziwafikie kwa kutumia mjadala husika kutueleza kwa kirefu walivyoweza kuvitambua, kuvilinda na kuviendeleza vipaji vyao. Je wewe umekwisha kijua kipaji chako? Unakikilinda na kukitetea?
Shukrani za pekee zimuendee ndugu Zito Kabwe kwa kuhudhuria mjadala baada ya kuliona tangazo letu mtandaoni. Kwetu vijana, umetuachia funzo kwamba yanapokuja masuala ya maslahi kwa umma kama haya ya uhamasishaji usomaji wa vitabu, viongozi nao wanajukumu kubwa.
Kwa hakika, mjadala wetu ulifana kutokana na mchango wa wasanii. Tunawashukuru mwanamuziki Vitali Maembe, Mwana-Hip Hop Danny Sepetu na mshairi Kezia . Ahsanteni sana!
Pia, tutakuwa wachoyo wa fadhila bila kumshukuru 'patner' wetu kwenye harakati za kuhamasisha usomaji wa vitabu Mama Demere Kitunga wa Soma Book Café ambaye tuliandaa naye tukio hili. Tusonge mbele Mama!
Mchoraji James Gayo alitupatia majarida ya Kingo ambayo tuliyagawa kwa wahudhuriaji. Shukrani sana ndugu!
Mwisho, tunawashukuru makomredi wetu wote waliotusaidia kufanikisha tukio letu kwa hali na mali. Bila nyinyi, hakuna 'Kitabu Nilichosoma'!
Tuendelee kukienzi kitabu. Chambilecho Betroit Bretch kwenye shairi lake la Praise of Learning (Tafsiri ni yetu):
“Tukuza kujifunza, Ewe utetemekae
Kifikie kitabu, Ewe mwenye njaa,
Kitabu ni Silaha!
……………….
Ado Shaibu
Seif Abalhasan
Diana Kamara


MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Mjumbe, leo nimetembelea blog yaku na kujikita hapa kwa muda. Shukrani sana kwa kuzipa nafasi kazi za KITABU NILICHOSOMA. Pia hongera kwa kuelimisha jamii kupitia blog yako.

    ReplyDelete

 
Top