SIKU chache baada ya uongozi wa jiji la Mbeya kutoa tahadhari juu ya
uwepo wa nyoka mkubwa aina ya chatu katika eneo la Rift Valley lililopo
pembezoni mwa mto Meta jijini humo chatu mtoto amekamatwa na kuzidisha
tishio la nyoka huyo FikraPevu imefahamishwa.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa tahadhari
ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya, Mei 14, 2014
kuwatahadharisha wananchi juu ya uwepo wa chatu huyo ambaye amekuwa
tishio kwa wakazi wanaofanya shughuli mbalimbali karibu na mto Meta.
Taarifa kutoka mkoani humo zinasema zoezi la kumtafuta nyoka huyo
zilianza Jumatatu Mei 19, 2014 sikihusisha wataalamu wa Wanyamapori
pamoja na waganga wa jadi ambao walikuwa wakimtafuta pembezoni mwa mto
huo.
Tangazo lililotolewa na Halmashauri Mbeya
Juhudi hizo zilianza kuonyesha mwanga asubuhi ya Jumatano Mei 20, 2014
wakati waganga wa jadi walipofanikiwa kumpata chatu mdogo pembezoni mwa
Mto Meta karibu na Hoteli ya Rift Valley.
Mganga wa jadi, Mazoea Hamis (39) mkazi wa Chalinze mkoa wa Pwani, alisema siku ya kwanza ya zoezi hilo walifanikiwa kugundua njia aliyokuwa amepita chatu huyo lakini hawakufanikiwa kumpata hadi jana walipofanikiwa kumpata chatu mdogo.
“Jioni yake baada ya kupumzika tuliona tuweke dawa za kienyeji ambazo zingiweza kumtoa mafichoni na kusogea karibu ambapo asubuhi jana tuliwahi kufika katika eneo hilo na kuendelea kumtafuta na bado tunaendelea kumtafuta” alisema Hamis.
Mganga wa jadi, Mazoea Hamis
(39) mkazi wa Chalinze mkoa wa Pwani aliyevalia nguo nyekundu zote,
akiwa na Athman Keneth (30), mkazi wa Chunya mkoani humo ambaye
anamsaidia ili kumpata chatu huyo
Alisema kwa kawaida chatu mdogo
anapoonekana, mkubwa anakuwa anahama ili kuwapisha wadogo kuendelea na
maisha yao au kwa namna moja au nyingine kusombwa na maji katika kipindi
cha mvua kutoka kwenye hifadhi zao pamoja na wengine
Taarifa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji zinadai kuwa, baada ya kukamatwa kwa chatu huyo atahifadhiwa na kutunzwa katika Hifadhi ya Wanyama ya Ifisi ambako kuna wanyamapori wengine kwa ajili ya maonyesho.
MJUMBE Sr
Post a Comment