Mtalii huyo Scott Brierley, 23 amesena kuwa amekuta picha ya Tembo wa Afrika katika simu yake baada ya kuwa imerudishwa na walinzi wa mbuga ya Safari aliyokwenda kutembea Magharibi wa Midlands karibu na Bewdley huko Worcestershire nchini Uingereza.
Mlinzi mkuu wa mbuga hiyo Andy Plumb amesema picha hiyo ni ya kwanza kabisa kwa mbuga hiyo.
Bw. Brierley amesema kuwa anaamini hiyo ndio Selfie ya kwanza kabisa duniani ya Tembo.
Amesema alikuwa amekaa ndani ya gari ambapo simu yake ikaanguka chini wakati akiwa anapiga picha ambapo simu hiyo ikabonyezwa na tembo aliyejikuta amejipiga Selfie kabla ya kuokotwa na walinzi ikiwa na picha hiyo.
MILLARD AYYO
Post a Comment