Unknown Unknown Author
Title: MJUMBE BLOG:TUNA SOGEZA HUDUMA KARIBU NA JAMII:IME WAGHIRIMU MCHUNGAJI MGWABATI NA MWANAE NUSU SIKU KUKAMILISHA ONLINE ADIMISSION!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
 Pichani juu:Kutoka Kushoto ni Frank na Katikati ni Dkt Augustino na Mchungaji Mgwabati wakifuatilia Usajili wa Vyuo Mbalimbali Mtandaoni....
 Pichani juu:Kutoka Kushoto ni Frank na Katikati ni Dkt Augustino na Mchungaji Mgwabati wakifuatilia Usajili wa Vyuo Mbalimbali Mtandaoni.
   Pichani juu:Kutoka Kushoto ni Dkt Augustno Katikati ni Frank Mgwabati na Kulia Kabisa ni Mch.Mgwabati Mwenyewe akifuatilia Mchakato Mzima.
    Pichani juu:Kutoka Kushoto ni Frank Mgwabati Katikati ni MJUMBE Sr Kulia Kabisa ni Mchungaji Mgwabati akishiriki Neno kwa Neno,Tungo kwa tungo na Aya kwa Aya ili kufanikisha Usajili wa Mwanae.


Changamoto kubwa katika Vijiji vingi nchini ni Mtandao wa internet kuwa dhaifu ama kuto kuwepo kabisa.
Timu yetu ya MJUMBE BLOG ni Sehemu ya Jamii hiyo,kwahiyo tuna guswa na kuathiriwa moja kwa moja na dhahama hiyo.Pamoja na Changamoto nyingi zinazo ikabili kazi yetu bado hatuja choka kutafuta na hata kudadisi ili Tufikie MALENGO yetu na Kusogeza japo kwa Hatua Moja Maendeleo ya Jamii na Taifa kwa Ujumla wake.

Sikupenda Kuliongelea hili mahali hapa lakini kwa sababu ime nilazimu ngoja niweke wazi hili;Kuna mengi ya Kujifunza hapa! Uvumilivu kwa wahusika walio jaribu kudadisi na kujua wapi unaweza pata huduma za Mtandaoni,Kwani ni wana nchi wangapi wame funga safari na hata wengine tumewahi diriki kuomba Ruhusa makazini ili tuka jifanyiea Usajili Mjini!Lakini Sisi Tume amua kuachana na utamaduni wa kuishi kwa mazoea Tuna amini katika kujaribu na Kuthubutu na ndio maana leo hii Tume weza kupata eneo amabalo uki kaa unaweza ukafanya shughuli zako mtandaoni huku kijijini.
Zaidi ya yote Niseme tu Nime upenda sana Utaratibu wa Mchungaji Mgwabati na Mwanae,Utaratibu wa Kufanya kazi Bega kwa bega na mwanae! Watoto wangapi leo wanatamani sana Siku moja kama hii Waongozane na baba zao Lakini Wameishia Kuambiwa Mimi nipo bize na kazi zangu! Tofauti na Mchungaji Mgwabati ameamua kuutoa Muda wake wa Thamani na Kutanguzana na Mwanae ili ahakikishe Anakamilisha Zoezi la Kujisajili.
Nifaraja iliyoje? Nimefarajika sana!

Sina Mengi zaidi ya Hayo;Pindi Upatapo Ujumbe Huu;Wasalimie Huko Mjini.Wambie Nilifika Salama!

Asante za pekee kwa Mpiga Picha wetu.

Wenu awapendae
MJUMBEanaye ishi Kijijini.
NJOMBE/LUDEWA
AMANI

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top