Wakati
Mwenge wa Uhuru ukizua mvutano mkali bungeni, Dodoma kiasi cha Waziri
Mkuu Mizengo Pinda kusimama na kutoa ufafanuzi, ujio wa Mwenge huo
wilayani Mbozi mkoani, Mbeya umesababisha mahabusi waliokuwa wakisubiri
kupelekwa mahakamani jana kukosa gari kwa madai liko kwenye ziara ya
Mwenge huo.
Mwendesha
Mashtaka wa Polisi, Joel Mori alisema mahakamani kuwa sababu za kukwama
kwa mahabusi kusomewa mashtaka juzi na jana ni ukosefu wa gari, ambalo
kwa sasa linafanya kazi za Mwenge.
"Sababu ni uchache wa magari ya kubeba mahabusi, lililokuwa likitegemewa liko kwenye ziara ya Mwenge iliyoanza Mei 26," alisema.
Aliiomba
mahakama kupanga tarehe nyingine ya kusikiliza kesi na Hakimu Nemes
Chami, alisema kesi hizo zitasikilizwa Juni 9, mwaka huu.
Wabunge Dodoma
Katika
kipindi cha maswali na majibu juzi wabunge wa upinzani walisimama wote
kupinga mbio za Mwenge kwa madai hazina tija. Juzi, Pinda alitoa
ufafanuzi kuwa hakuna dhambi kwa Mwenge kuendelea kukimbizwa nchini kwa
kuwa unaimarisha uzalendo.
Na Martha Magesa
MJUMBE Sr
Post a Comment