Naibu waziri wa fedha Tanzania ambaye pia ni Naibu katibu mkuu wwa CCM Tanzania bara Mh Mwigulu Lameck Nchemba akihutubia wakazi wa Iringa.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano huo

kushoto ni katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga, Kulia ni mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christina Ishengoma akiwasalimu wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.

Wananchi wa mkoa wa Iringa wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa

Mh Mwigulu Nchemba akihutubia

Mwenyekiti wa chama CCM mkoa wa Iringa Bi Jesca Msavatavangu akizungumza katika mkutano huo.

Wananchi wakimsikiliza Naibu waziri wa fedha Mh Mwigulu Nchemba

Naibu waziri wa Maendeleo, Jinsia na watoto Mh Pindi chana akizungumza katika mkutano huo

Na Mathias Canal(IRINGA)
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeendela na mikutano yake ya kukiimarisha chama kwa kuwafafanulia baaadhi ya mambo ambayo wapenzi na wanachama wa chama hicho wamekuwa wakipotoshwa na baadhi ya vyama.
Akifungua mkutano huo iliofanyika hii leo katika viwanja vya Mwembetokwa Manispaa ya Iringa, mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Iringa Bw Abed Kiponza amewapongeza watu waliojitokeza katika mkutano huo na kusema kuwa chama hicho kitaendelea kuwa imara na kupata kura nyingi kwa kuwa Watanzania bado wana imani kubwa na chama hicho.
Naye katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bw Hassan Mtenga amesema kuwa huu sio muda wa Watanzania kudanganywa na vyama vya upinzani kwani chama tawala ndicho chenye nguvu ya maamuzi ya kujenga shule,zahanati na barabara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Bi Jesca Msavatavangu amewapongeza wananchi waliojitokeza na kusema kuwa mapambano bado yanaendelea, na mwaka 2015 vyama vya upinzani haviwezi kuambulia jimbo hata moja la uchaguzi katika mkoa huo.
Naye mgeni rasmi katika mkutano huo Mwigulu Lameck Nchemba ambaye ni Naibu Waziri wa fedha Pia ni Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara amesema kuwa tatizo kubwa linalowakabili watanzania sio katiba mpya bali ni upungufu wa ajira.
Hata hivyo Nchemba amesema kuwa na serikali tatu kwenye katiba mpya ni jambo ambalo haliwezekani kwani kukiwa na kukiwa na serikali tatu kutakuwa na gharama kubwa ya kuendesha serikali hizo kwa kutumia fedha inayotoka kwenye kodi ya wananchi.

Aidha ameongeza kuwa jambo la katiba halikuwepo kwenye ilani ya CCM lakini vyama vya upinzani ndivyo vilivyoibua hoja hiyo ambayo imewashinda kwa kutoka bungeni mara kwa mara.
Nchemba amesema anawashangaa wale wanaosema ana mawazo ya kimasikini na kukiri kuwa amekuwa na mawazo ya kimasikini kwa kuwa rafiki zake ambao ni Watanzania ni masikini.
Sambamba na hayo Nchemba amesema anapeleka sheria bungeni itakayofuta kodi kwa wafanyabiashara ndogondogo kwani nchi ya Tanzania imekuwa ikiendeshwa kwa kodi za wafanyakazi na wafanyabiashara ndogondogo.

Post a Comment