Pichani Juu Ni Moses Mgallah akiwa hutubia wana nchi wa Mlowo Jioni ya leo
Pichani juu ni Mkisi ambaye alijitambulisha kama moja kati ya wanajopo wanao fanya Utafiti wa Sera za Chama Nyanda za Juu Kusini akitoa Sera zake kwa Wananchi wa Mji Mdogo wa Mlowo jioni ya Leo.
Pichani juu ni Shombe Fadhiri aliye jitambulisha kama Mwanasheria wa CHADEMA Nyanda za juu kusini akitoa nasaha kwa wapiga kura watarajiwa wa Mji mdogo wa Mlowo,Mbozi jioni leo.
Paschel Haonga,Akinukuu moja ya Ibara za Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ili kuthibitisha anacho kiamini na anachotaka Wana nchi wa Mji Mdogo wa Mlowo Waelewe kuhusu Mwenendo mzima wa nchi.
Pichani juu ni Diwani wa Mji Mdogo wa Tunduma akihutubia katika mkutano wa Hadhara Ulio fanyika Leo Katika Mji Mdogo wa Mlowo.
Pichani juu ni Sebastian Kilindu alimaarufu kama Seba ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya akikanusha uvumi kuwa Alihongwa ili ahame Chama na Kuwa Chama kime mfukuza uenyekiti wake.
Pichani juu ni Jidawaya S Kazamoyo akiendelea kutoa sera na hoja zake kuhusu hatima ya Machaguo wanayo yafanya wana nchi na Mstakabali wa Nchi kwa Ujumla.
Jambo lingine Lililo Ongelewa karibu na Kila Muongeaji ni suala la Ushuru wa Mageti unao onekana kuwa Kukwazo kwa Wakulima na Umeongeza Gharama zaidi.Hapa waongeaji wote wali lalamikia suala la Mageti ya Ushuru yanayo onekana kugeuzwa kama chanzo cha Kujiingizia Kipato kwa Wahusika.
Suala la Ushuru wa Soko la Mlowo pia lilionekana kupigiwa Chapuo na Mhe.Diwani wa Mji mdogo wa Mlowo amabye alieleza kuwa Mpango wa Serikari na Aliye pewa Tenda ya Kukusanya Ushuru ndani ya Soko kuu la Mlowo ili kuwa ni kukusanya Sh.Milion Hamsini kwa Mwaka wakati Tangu afukuzwe na Kupewa Usimamizi kwa wanachi Wamesha Kusanya Zaidi ya Milion Mia mbili Suala amabalo lime changia kupunguza Michango kwa Wananchi na Wakazi wa Mji Mdogo wa Mlowo kwani Huduma za Jamii Kama Shule Zime Jengwa Kwa kutumia asilimia Ishirini toka Ile iliyo patikana kwenye Kusanyo la kodi jambo lililo onesha kuwa Furahisha zaidi wasikilizaji.
Taarifa Zote Na Picha Na Mpiga Picha Wetu wa Kujitolea @Sr
MJUMBE Sr
Post a Comment