Mwanamke raia wa Sudan
aliyesamehewa adhabu ya kifo baada ya kubadili dini amesafirishwa hadi
nchini Italia baada ya kuwa kwenye ubalozi wa Marekani mjini Khartoum
kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Meriam Yahia Ibrahim Ishag na familia yake
waliondoka na ndege ya serikali ya Italia wakiongozana na Waziri wa
nchini Italia Lapo Pistelli.Meriam mwenyewe alilelewa na mama yake ambaye ni mkristo na kusema kuwa hajawahi kuwa muislamu.
Mume wa Meriam Daniel Wani, ni mkristo,ana asili ya Sudani kusini na ana uraia wa Marekani.
Mtoto wa Meriam, Maya alizaliwa gerezani mwezi May, muda mfupi baada ya kuhukumiwa kunyongwa hatua iliyosababisha ghadhabu dunia nzima.
Aliachwa huru mwezi Juni baada ya kuwepo kwa mashinikizo.
BBC SWAHILI
Post a Comment