Unknown Unknown Author
Title: JKT:YAKANUSHA KUWA VIJANA WANAKUFA KWA UKATILI JESHINI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TANGAZO JESHI LA KUJENGA TAIFA, LINAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KWA KUTUMIA UJUMBE MFUPI WA MANENO (SMS) KATIKA SIMU ZA VIGANJANI NA M...
TANGAZO JESHI LA KUJENGA TAIFA, LINAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KWA KUTUMIA UJUMBE MFUPI WA MANENO (SMS) KATIKA SIMU ZA VIGANJANI NA MTANDAO WA JAMIIFORUM.COM, KWAMBA VIJANA WA KUJITOLEA NA MUJIBU WA SHERIA WANAOENDELEA NA MAFUNZO KATIKA MAKAMBI YA JKT WANAKUFA KWA UKATILI, WAKITOLEA MFANO KAMBI YA JKT OLJORO ARUSHA KWAMBA KUNA VIJANA WATATU WAMEFARIKI DUNIA.UMMA UFAHAMU KUWA TAARIFA HIZO SI ZA KWELI NI UPOTOSHAJI KWA VIJANA NA WATANZANIA. UKWELI NI KWAMBA KUNA KIJANA MMOJA WA KIKE HONORATA VALLENTINE OISO ALIYEFARIKI KATIKA KIKOSI CHA JKT OLJORO ARUSHA KWA UGONJWA WA UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA) ULIOSABABISHWA NA MALARIA. SIO VIJANA WATATU KAMA INAVYOELEZWA KWENYE UJUMBE UNAOSAMBAZWA. WAZAZI WA KIJANA ALIYEFARIKI PIA WALITHIBITISHA KUWA KIJANA WAO ALIKUWA NA MATATIZO YA UPUNGUFU WA DAMU. JESHI LA KUJENGA TAIFA LINASISITIZA KUWA HAKUNA UKATILI WOWOTE UNAOFANYWA KWA VIJANA WANAOENDELEA NA MAFUNZO KATIKA MAKAMBI YA JKT. JKT LINALAANI KITENDO HICHO NA LINAFUATILIA ILI KUBAINI CHANZO CHAKE. MTU YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUWA NDIYE CHANZO CHA UJUMBE HUO, HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.JESHI LA KUJENGA TAIFA LINAWAKUMBUSHA VIJANA NA WATANZANIA KUWA MAKINI NA MATUMIZI MABAYA YA SIMU ZA MIKONONI NA MITANDAO YA JAMII, HASA KWA TAARIFA ZINAZOHUSISHA JESHI. TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JKT. MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top