Unknown Unknown Author
Title: KUHUSU ALIYETUNGUA NDEGE YA ,MALAYSIA,URAIA WA ABIRIA NA TAMKO LA OBAMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Tukio la kudunguliwa kwa ndege ya Malaysia Boeing 777 katika mpaka wa Ukraine na Urusi limeshtua dunia kwa mara Ya pili ikiwa ni miezi...
Tukio la kudunguliwa kwa ndege ya Malaysia Boeing 777 katika mpaka wa Ukraine na Urusi limeshtua dunia kwa mara Ya pili ikiwa ni miezi minne tangu ndege nyingine ya Malaysia ipotee na hadi sasa haijapatikana.
Waziri mkuu wa Malaysia, Naji Razak ameliita tukio kuwa ni tukio la kusikitisha sana na la kushitua huku akisisitiza kuwa uchunguzi utakaofanyika juu ya tukio hilo usikumbwe na kikwazo chochote.
Idadi ya watu waliokuwa kwenye ndege hiyo iliripotiwa kuwa 195 awali, imethibitika kuwa ni watu 198 hivi sasa huku zaidi ya miili 100 ikiripotiwa kupatikana.
Shirika la ndege la Malaysia limeeleza kuwa ndege hiyo likuwa imebeba raia 154 wa Uholanzi, 27 wa Australia, 43 wa Malaysia ikiwa ni pamoja na wafanyakazi 15, raia 12 wa Indonesia na tisa wa Uingereza.
Abiria wengine wametajwa kuwa wajerumani, Wabelgiji, wafilipino, wacanada huku wengine 41 hawajathibitishwa uraia wao.
Ukraine na Urusi wote wamekana kuhusika na shambulio la ndege hiyo ya abiri huku hisia kubwa ikipelekwa kwa waasi wa Ukraine kwa kuwa ndege hiyo imedondoka katika sehemu ya ardhi wanayoithibiti.
Rais wa Marekani, Barack Obama amelitaja tukio hilo kuwa tukio la kusikitisha sana na kwamba bado hajafahamu kama kuna raia wa Marekani aliyekuwa kwenye ndege hiyo.
“Mawazo yetu na maombi yetu ni yako na familia za abiria, kokote watakapopaita nyumba.” Alisema Obama.
Hata hivyo, ikulu ya Marekani imewatetea waasi wa Ukraine kufuatia tukio hilo wakidai hawakuwa na uwezo wa kufanya shambulizi hilo kwa kuzingatia umbali wa Kilometa 10 iliporuka ndege hiyo.
Taarifa zilizopatikana hivi punde zinaeleza kuwa kifaa kinachorekodi taarifa za ndege hiyo ‘black box’ kimepelekwa Moscow kwa uchunguzi.
Viongozi wa nchi mbalimbali duniani wameendelea kutuma salamu za rambirambi kwa Malaysia kufuatia tukio hilo.
Chanzo:Times Fm


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top