MAJANGA PLUS YA LUDEWA:ULANZI LITA MBILI TSH.2000;BEI YA MAHINDI DEBE MOJA NI TSH.3000! WAKULIMA WAHAHA... SOKO HAKUNA!
Mpaka sasa wakulima Wilayani Ludewa hawijui nini hatima yao ya Mazao ambayo mengi bado yapo shambani kutokana na Kukosa soko la uhakika,jambo lililo zua minong'no kwa wakulima na kuendeleza sintofahamu ya nini Mpango wa Serikari kwa Mazao yao hasa ikizingatiwa Mpaka hivi sasa ime funga mipaka kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi kuingia na kufanya biashara jambo linalo endelea kuwa umiza wakulima walio wengi ambapo mpaka sasa Mfumko wa Bei ya bidhaa mbali mbali umekua mkubwa ikilinganishwa na Zao la Mahindi ambalo ndilo limekua Zao la Biashara na Tegemezi Miongoni mwao,kwani mpaka sasa Bei wanayo uzia kwa Walanguzi ni Tsh.3000 na Haijulikani wala hakuna Taarifa Rasmi kutoka Serikarini ya Lini Bei ama Soko Litafunguliwa Rasmi,Jambo ambalo lime endelea Kuwa umiza wakulima na kuwa fanya waishi maisha ya tabu Mno kwani Gharama ya uzalishaji io juu sana Ikilinganishwa na Bei ya Mazao hayo.
Pichani ni Moja ya Kijiwe cha walanguzi kama kilivyo naswa na Kamera yetu siku chache zilizo pita Mtaani Kijijini Amani,Ludewa
Tofauti ilivyo kwa Bei ndogo ya Mahindi katika Wilaya ya Ludewa,mpiga picha wetu amekutana na kali ya mwaka Baada ya Kubaini kuwa Pombe aina ya Ulanzi lita mbili ina kimbizana Bei na Debe moja la Mahindi kwani Mpaka sasa Bei ya Lita Mbili ya Ulanzi ni Tsh 2000 Ikilinganishwa na Mahindi debe moja ambalo ni Tsh.3000 tu.
Wakiongea kwa Nyakati tofauti Wakulima wa Zao la Mahindi Kijijini Amani walio onesha kukatishwa tamaa na Bei za Mahindi zinazo endelea Kuwa umiza na Imebainika kuwa Wakulima mpaka sasa hawana Chagua Mbadala kwa Soko la Mahindi yao na hivyo wengi wao Wame amua kujitosa na Kuuza kwa Bei hiyo ili tu wanusuru mengine mengi ambayo yapo Shambani.
Milonjo Mtitu,alisema "....Saizi kwetu ni kilio.. bora wafanyakazi... Mahindi yapo shambani.. wavunaji nao wamesha maliza kazi zao.. wanadai Pesa yao na Bei haieleweki..."
Mkulima Mwingine aliye julikana kwa jina Moj a tu la James alisema "Serikari ndio ina tuumiza.... kwani Imefunga mipaka lakini Haina uwezo wa kuja kumaliza Mahindi kwa wakulima hata ingefanaje Mahindi huko mashambani ni mengi mno... na mwaka huu lazima Tuumie"
Hayo ni miongoni mwa yanayo endelea kuongelewa kuhusu Soko la Mahindi linalo onekana kuzidiwa sipidi siku hadi siku Wilayani Ludewa.
Maelezo Yote na Picha Kwa Hisani ya Mpiga Picha Wetu wa MJUMBE BLOG.
Post a Comment