Marekani na Ujerumani zimetaja kitendo hicho kama hatari na kwamba kuna hofu huenda Urusi ikatumia hatua hiyo kama sababu ya kuivamia Ukraine.
Awali NATO ilikuwa imesema kuwa Urusi inasafirisha silaha kali kuingia nchini Ukraine na kwamba imekuwa ikitumia mizinga yake ndani ya ardhi ya Ukraine dhidi ya vikosi vya Ukraine.
Hatahivyo Urusi inasema kuwa msafara huo umebeba maje-nereta, chakula na maji,lakini waandishi walioona malori hayo wanasema kuwa yamebeba mizigo nusu na kwamba Ukraine inasema kuwa msafara huo unatumiwa kuwasaidia waasi wanaounga mkono Urusi katika eneo la mashariki.
BBC SWAHILI
Post a Comment