Unknown Unknown Author
Title: MTENDAJI MKUU WA KAMPUNI YA APPLE AME JITANGAZA KUWA NI SHOGA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Apple, Tim Cook jana amejitangaza kuwa yu shoga; “Wacha niseme wazi, najivunia kuwa shoga na nachukulia ushoga ...
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Apple, Tim Cook jana amejitangaza kuwa yu shoga; “Wacha niseme wazi, najivunia kuwa shoga na nachukulia ushoga wangu kama zawadi muhimu sana ambayo mungu amenipa……..wafanyakazi wengi wa APPLE wanajua mimi ni shoga na haioneshi tofauti yoyote kwa namna wanavyofanya kazi nami” SOMA ZAIDI MAONI YA MTATIRO MAANDIKO YANASEMA NINI KUHUSU USHOGA? Warumi 1:26-27 "Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasio ya asili wanaume nao vivyo hivyo, waliyaacha mtumizi ya mke, ya asili wakawakiana tama wanaume wakayatenda yasiyopasa wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao." JE! MAPENZI YA NAMNA HII NI DHAMBI? Imeandikwa, Mambo ya walawi 18:22 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke ni machukizo." JE ANAYEFANYA MAPENZI YA NAMNA HII ATAURITHI UZIMA? Imeandikwa, 1Wakorintho 6:9 "Au hamjui yakuwa wadhalimu hawatauridhi ufalme wa Mungu wala wabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti." Je wanaweza kutubu na kusamehewa? Imeandikwa, 1Timotheo 1:10-11 "Na wazinzi, na wafiraji, na waibao watu, na waongo nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana mafundisho yenye uzima, kama vile ilivyo nenwa katika habari njema ya utukufu wa Mungu ahidimiwaye, niliyowekewa amana." Imeandikwa, 1 Wakorintho 6:11 "Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii, lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu." JE! KAMA UNAFANYA MAPENZI YA NAMNA HII UFANYE JE?. Kwanza, kubali dhambi zako. Imeandikwa, Zaburi 51:2-4 "Unioshe kabisa na uovu wangu unitakase dhambi zangu... maana nimeyajua mimi makosa yangu " Pili, omba msamaha kwa Mungu na kutorudia dhambi hizo. Imeandikwa, Zaburi 51:7-12 "Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko theluji unifanye kusikia furaha na shangwe mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; uzifute hatia zangu zote. Ee Mungu uniumbie moyo safi, uifanye upia roho iliyotulia ndani yangu. Usinitenge na uso wako wala Roho yako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako unitegemeze kwa roho ya usafi." Tatu, kubali ya kuwa Mungu amekusamehe dhambi zako. Imeandikwa Zaburi 32:1-6 "Heri aliyesamehewa dhambi, na kusitiriwa makosa yake. Heri Bwana asiyemhesabia upotovu,, ambaye rohoni mwake hamna hila. Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea. jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi. Nalikujulisha dhambi yangu wala sikuufisha upotovu wangu nalisema nitayakiri maasi yangu kwa Bwana nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu. Kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana, hakika maji makuu ya furikapo hayatamfikia yeye." Kama umesoma na kuelewa ujumbe huu, gonga “AMINA” au “WEKA MAONI YAKO”. J. Mtatiro, Dar Es Salaam.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top