es Salaam. Askofu Msaidizi wa Jimbo la
Bukoba, Methodius Kilaini amekiri kupokea
Sh80.5 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa
VIP Engeering, James Rugemalira akisema si
mara yake kwa kwanza kupokea fedha kutoka
kwa mfanyabiashara huyo kwa kuwa mara
nyingi huwa anachangia kwa uwazi miradi ya
jamii.
Askofu huyo alikuwa akizungumzia Ripoti ya
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),
iliyosomwa bungeni juzi ikimtaja kuwa ni
miongoni mwa viongozi wa dini na watu
wengine waliopokea mabilioni kutoka katika
akaunti ya escrow.
Katika ripoti hiyo, Zitto aliwataja viongozi
wengine wa dini walioingiziwa fedha katika
Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa
Katoliki kuwa ni Askofu Eusebius Nzigirwa
(Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimanye
Simon (Sh40.4 milioni).
Akizungumza kwa simu jana, Askofu Kilaini
alisema Rugemalira hupendelea kuchangia
kwa uwazi miradi ya kijamii na si yeye peke
yake aliyempatia mchango, bali kuna watu
wengine wengi ambao wameshampatia na
kazi yake ni kuipokea na kuifikisha sehemu
husika.
Hata hivyo, kabla hajafafanua zaidi hoja yake,
simu ilikatika na baadaye hakupatikana tena.
Hata hivyo, jana askofu huyo alinukuliwa na
Gazeti la Mawio toleo la jana akisema fedha
alizozipokea kutoka kwa Rugemalira ni kwa
ajili ya miradi mbalimbali inayoendeshwa na
Kanisa Katoliki.
“Ndiyo nimepokea fedha kutoka kwa James na
hii siyo mara ya kwanza, kwani mara nyingi
amekuwa akichangia miradi mbalimbali ya
kijamii,” alisema Askofu Kilaini.
Alipotakiwa na gazeti hilo kuwataja wengine
waliochangia kanisa lake na kama nao
wamechanga kutoka kwenye fedha za akaunti
ya escrow, alisema yeye hayumo kwenye
michango hiyo.
Alipoulizwa anawezaje kusema hayumo
kwenye orodha ya waliopewa fedha kutoka
akaunti ya escrow wakati anakiri kuwa
aliingiziwa mamilioni ya shilingi na
Rugemalira, alisema michango inayoletwa
kwake haina siri, hivyo wezi halisi ndiyo
wakamatwe.
“Michango inayoletwa kwangu haina siri,
shikeni wezi halisi,” alisema.
Askofu Nzigirwa
Kwa upande wake, Askofu Nzigirwa ambaye
alirithi kiti cha Kilaini, cha Askofu Msaidizi
Jimbo Kuu la Dar es Salaam ameeleza
kushtushwa kwake na ripoti ya PAC iliyomtaja
yeye na Kilaini kuhusika katika uchotwaji wa
Sh306 bilioni za escrow.
Rejea:Mwananchi
LIKE page yetu MJUMBE BLOG au Tutembelee Mtandaoni andika MJUMBE BLOG kisha ingia hapo.
©Mjumbe Blo
Post a Comment