Habari wakuu,
Leo ni mdahalo unaoendeshwa na mfuko wa
mwalimu Nyerere kuhusu umuhimu wa
kuzingatia mambo ya msingi sasa katika katiba
iliyopendekezwa ya Jamhuri ya muungano wa
Tanzania.
Wahusika
Jaji Warioba (Aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya
katiba)
Joseph Butiku (Mkurugenzi mtendaji mfuko
Mwalimu Nyerere)
Mwantumu Malele (Mtumishi wa umma
mwandamizi msataafu)
Palamaganda Kabudi (Mhadhiri mwandamizi
UDSM)
Awadhi Ali Saidi (Raisi wa chama cha
wanasheria Zanzibar)
Humphrey Polepole(Aliyekuwa mjumbe bunge la
katiba)
Moja kwa moja kutoka ukumbi wa mikutano wa
Mlimani city kupitia JamiiForums kuanzia saa
Tisa
==============================
===================
Muongozaji wa mdahalo ni Hamza Kasongo na
ndiye alianza kuongea sasa na anaelezea
midahalo iliyopita ukiwemo ulioleta vurugu,
anaelezea watakaoongea mdahalo wa leo na
ratiba yake kwa ujumla mwisho anamkaribisha
Joseph Butiku
JOSEPH BUTIKU
Mdahalo huu ni muendelezo wa mdahalo wa
tarehe mbili uliokubwa na vurugu, anasisitiza
amani itawale kwenye mdalaha, heshima na
uhuru wa mawazo, hoja makini na watu
wafatilie badala ya kupoteza muda. Hayo ndio
msingi wa taasisi. Msingi huu alituachia baba
wa taifa kuhahakikisha nchi inabaki katika
amani na umoja. Tanzania imesaidia wengi
kupata uhuru wao(anazitaja nchi) na kiasi
kikubwa cha damu zilimwagika ili wahusika
wapate uhuru. Taifa letu halibaguani na
tulisaidiana na wote kuleta uhuru, Tumshukuru
Raisi Kikwete kwa kuacha uhuru huu na mtu
anaegombana hana hoja. Tunakubaliana na
tusipokubaliana tunatoka nje. Anamkaribisha
ndugu Warioba kuielezea katiba
inayopendekezwa. Kutakua na mada wa
maswali na kupata ufafanuzi.
JAJI WARIOBA
Mdahalo huu ni muendelezo, nitarudia kwa ufupi
niliyosema tarehe mbili. Nilianza na utaratibu
wa kura ya maoni na unaongezwa na sheria ya
kura ya maoni. Hatua ya kupiga kura ya maoni
inaongozwa na sheria ya kura ya maoni.
Anashukuru raisi amepata matibabu na afya
yake inaimarika na anamuombea apone haraka
kwa sababu ya jukumu lake la kuongoza nchi
hii.
Raisi alieleza utaratibu mzima na aliainisha
kufika mwisho wa march mwakani tume ya
uchaguzi itakua imekamilisha daftari la wapiga
kura. Katiba ile inatakiwa miezi miwili kwa ajili
ya elimu kwa umma kwabla ya kampeni kuanza.
Lengo la mchakato huu ilikua tupate katiba
ambayo itakua tofauti na katiba ya sasa na
wananchi walitoa maoni. Tuone maoni
yaliyopendekezwa mabadiliko ni yapi ili tuwe na
katiba tofauti.
1.Wananchi walitoa maoni mengi sana kuhusu
dira ya taifa, ni muhimu katiba ionyeshe dara ya
taifa kama wakati wa azimio la Arusha. Katika
katiba ya sasa tunayo malengo katika ibara ya
nane(siasa ya ujamaa na kujitegemea) lakini
ilikua finyu sana
Kwanza kuwe na lengo kuu linalotuonyesha
tunaenda wapi na lengo kuu likawa kulinda na
kudumisha umoja, amani(anasema mengi) ya
wananchi. Katika katiba inayopendekezwa
ilifafanua katika kila kipengele tofauti na katiba
ya sasa inayoelezea kwa ujumla tu. Bunge
maalumu kwa ujumla limepitisha haya. Lakini
ilivyopitishwa kuna kasoro mbili. Moja
hayatakua na nguvu la kisheria na wameingiza
mambo yasiyohusu dira mfano taasisi ambayo
ipo kwenye uendeshaji. Pili haki za binadamu,
haki tulizonazo kwenye katiba nyingi zilikua na
vikwazo na zipo ambazo hazikuwemo katika
katiba na sisi tuliziweka zote na bunge
lilizingatia na kuboresha. Tatizo, kufuatana na
maoni ilikua haitoshi tu kuorodhesha haki bila
utekelezaji. Bahati mbaya bunge maalumu
waliliondoa hasa kwa makundi madogo,
wameweka pia kutegemea uwezo wa kitaifa.
Madaraka ya raisi, asiwe na madaraka kila
mahali, pili ktk nafasi nyeti raisi apate ushauri
katika kuteua mfanu tume ya uchaguzi na yote
wameyapitisha, tatu baadhi ya vyeo apate
ridhaa ya umma lakini hili wamelikaa kinyume
na dunia wanavyofanya kwa sasa.
1.Maadili yameporomoka sana katika nchi hii
hivyo wananchi walisema iwepo sura
inayozungumzia maadili na kuwepo na tume
(anazitaja anazozikumbuka). Bunge maalumu
wameacha tu utu na lugha mengine yote
wameondoa.Tume ilipendekeza kanuni na miiko
ya uongozi. Hii ni misingi ya kitaifa na sio ya
uongozi pekee na yameondolewa na bunge.
Wanasema haya yanafaa yaende kwenye sheria
kinyume na maoni ya wananchi na utafiti
waliofanya.
Israeli Ikijulikana una akauti nje haina haja ya
TAKUKURU, unawajibika hapohapo. Kuna wakati
Mwalimu alishauriwa awe na akauti nje, sio tu
alikataa lakini aliitoa ile barua nje na kuikemea.
Kiongozi ana sababu gani kuwa na akaunti nje
zinufaishe nchi nyingine ila wamekataa isiwemo
kwenye katiba. Bunge litatunga sheria na
kuelezea tafsiri ya zawadi na masharti ya
kiongozi wa umma kufungua akaunti nje. Kwa
maana nyingine wamewaruhusu ila
wanawatengenezea utaratibu.
Lengine lilikuwa wawe(wananchi) waweze
kuondoa wabunge wao kama hawatoshi katika
nafasi zao. Kuna wabunge baada ya uchaguzi
wanapotea na kuna wale wanaoahidi mambo
mengi sana ambayo hawayatekelezi. Katiba ya
Kenya kifungu 104, wameruhusu kuondoa
mbunge. Huku vyama vinatuchagulia wa
kutuongoza, tuliweka 50-50 na kila jimbo litoe
wabunge wawili Mwanamme na mwanamke.
Mgombea binafsi wamemuwekea sheria, kwanini
masharti ya mgombea binafsi hayawekwi
kwenye katiba na kuacha ya wagombea kupitia
vya.
Tulitaka tutenganishe serikali na Bunge kwani
serikali linaminya uhuru wa bunge. Kinyume
chake pia bunge linaingilia kazi za serikali.
Tulipendekeza mikaba yote ipelekwa bungeni na
wamekataa hili. Mfano bunge kuamuru polisi
likamate watu ambayo ni kazi za serkali.
La mwisho muungano na Mohammed ataelezea
zaidi. Malalamiko ya serikali mbili, Kwanza
Tanzania bara imevaa koti la muungano kwa
miaka thelathini, tuliyarudisha baadhi ya mambo
ya muungano ikiwemo kodi ambalo liliondolewa,
Zanzibar walilalamika 1977 kwamba wao ndo
wanaendesha nchi(Zanzibar) lakini kodi
hawachukui na inachukuliwa na serikali ya
muungano.
Loans Board sio elimu ya juu ni facility tu ya
kuendesha elimu ya juu lakini vyuo vya Zanzibar
viko chini ya serikali Zanzibar.
Zanzibar wana mamlaka zao(anazitaja) na sasa
inajiita nchi, hivyo Zanzibar ibadili sheria zake
(anazitaja) mfano sheria ya ardhi na sheria ya
mkaazi. Haya kukubalika lazima kuwe na
maridhiano na haoni dalili ya maridhiano na
mchakato huu unaweza kuvunja umoja wa
kitaifa ambao angalau upo kwa sasa.
Nilivyosikia waheshimiwa wananitukana na
kubeza kama njia ya kupata ushindi, anasema
sio njia nzuri ila tuelimishane na mwisho
tutapiga kura hasa waheshimiwa
wanaoheshimika. Wanasema tunamsaliti
mwalimu, yeye alikua raisi lakini alipoona dalili
za ufisadi alipitisha azimio la Arusha akijua
linaanzia kwake. Mwalimu 1984 alikazana
tuweke ukomo wa uraisi wakati alikua raisi japo
alijua itaanzia kwake. Wanasema alitaka serikali
mbili lakini zilikua na mashati yake, mambo
waliyokubaana na Karume wameondoa katika
muungano, safari ya kutoka serikali mbili
kwenda serikali moja sasa imekua kinyume,
tumeondoa uhalali wa mwanzo.
Serikali isambaze nakala ya katiba
inayopendekezwa ili tujue tunapigia nini kura,
ASANTENI.
MUUNGANO(Mohammed Yusuph kutoka ZNZ)
Japo si mwanasheria nimejifunza sana sheria,
utafiti wangu mdogo kuhusu muungano wetu.
Nimeangalia vyanzo vingi kama katiba, hati ya
muungano, katiba inayopendekezwa NK
1.Jamhuri ya muungano
Hati ya muungano inasema ZNZ na Tanganyika
zinaungana kuunda jamhuri moja, katiba ya
1977 inasema kinyume na hati ya muungano
kuwa Tanzania ni nchi moja. Rasimu inasema
jamhuri ya muungano ni nchi moja lakini ni
shirikisho la nchi mbili. Katiba inasema (1+1)=1
hivyo inavunja makubaliano ya nyuma.
Muundo wa muungano ibara ya tatu na nne
(anazinukuu) katika hati ya makubaliano ya
muungano, anajiuliza baada ya miaka 50,
imekuwaje. Tanganyika iliyojivisha koti la
muungano ndio ina mamlaka ndani na nje ya
nchi. Tume ilipendekeza kuipatia Tanzania
katiba ya kweli lakini sasa wanatupa katiba ya
Tanganyika iliyofanyiwa marekebisho na
tunaipoteza fursa ya kipekee.
Ushirikiano ya kimataifa halikuwepo katika
orodha ya mambo ya kimuungano. Katiba ya
ZNZ iko kimya kwenye mambo ya kimataifa.
Ingawaje katiba inapendekeza lakini Zanzibar
itabakia sehemu ya Tanzania hivyo haitaweza
kujiunga katika taasisi yeyote ya kimataifa
kutokana na sheria zilizopo katika taasisi hizo.
Kuendelea kuchanganya mambo ya muungano
na yasiyo ya muungano kutaendelea kuvuruga.
Masharti ya mpito katiba ya jamhuri ya
muungano itakua katiba ya nchi, Pendekezo
linavunja masharti ya hati ya muungano.
Tumepata fursa ya kuandika katiba na
wananchi walipta fursa ya kuandika katiba
mpya pia kujijengea historia ya maisha yao
kutengeneza katiba, Maraisi ajiliulize kuwa
wamefikisha malengo ya kupata katiba kwa ajili
ya wananchi, tuombe tupate katiba nzuri na
kwa amani. ASANTENI SANA
Tofauti kubwa ya katiba iliyopendekezwa na
iliyopitishwa na bunge(POLEPOLE)
Tume ililenga kuleta katiba ya kimapinduzi
ambayo inaandikwa na wananchi wenyewe,
katiba ya kimapinduzi haiandikwi na viongozi
wala wawakilishi wa wananchi bali wananchi
wenyewe. Kuonyesha ukaribu wa wananchi na
serikali yao pamoja na mihimili yote. Raia
wanaweza kuwawajibisha viongozi wao moja
kwa moja. Kwa hali tuliyokuwa nayo tunahitaji
katiba ya kimapinduzi.
Kenya, Ujerumani, Taiwan, Argentina, Ecuador,
Finland n.k, wana ibara inayoweza
kumuwajibisha kiongozi.
Iweje Waziri awe na shahada na mbunge awe
na elimu ya Darasa la saba, wakati wote
wanatokana na bunge.
Wako maraisi wastaafu walitaka serikali tatu,
mengine tunaweka kifuani tu, wako mawaziri
wakuu walitaka serikali tatu kwenye kikao na
baraza la mawaziri. Wanasema rasimu haijataja
rushwa, haya hatufanyi kimuungano wakati
Zanzibar ina mamlaka yake ya kusimamia
rushwa(ZAREKA), TAKUKURU haivuki bahari.
Serikali haina sehemu hata moja, mchakato ni
wananchi na vyombo vyao, ni aibu mawaziri
kuipigia chapuo na kuishangilia katiba wakati
wanaosimamiwa ni wao wenyewe
Ibara ya 44 ya rasimu ya Warioba
inazungumzia vijana, anauliza ajira za vijana
zinaletwa na baraza la vijana mpaka
lilazimishwe kuwemo ndani ya katiba.
Wanawake ni wengi kuliko vijana mbona halimo
baraza lao kwenye katiba. Wako wawakilishi wa
watu wenye ulemavu lakini hawajachaguliwi na
walemavu. Bunge wamefuta kipengele cha
kuwashirikisha walemavu kupata viongozi wao.
Serikali imara kwa watendaji waandamizi,
tulipendekeza nafasi ya katibu mkuu kiongozi
athibitishwe bungeni lakini wamefuta, waweke
nafasi za makatibu wakuu wa wizara kwa
sababu ajira yao hazijalindwa na katiba hivyo
kufanya kazi kwa hofu za kisiasa lakini
wamefuta.
Sifa za kupoteza ubunge, kuumwa miezi sita
mfululizo, mbunge aache ili ahudumu afya yake
na akipona aombe awamu nyingine
Dedication mjadala wa Escrow, katiba ya
Warioba ilisema Likitokea tatizo kubwa la
uwajibikaji iliwekwa dhana ya collective
responsibility na walikifuta mwanzoni haraka
sana. Kiongozi wa umma akituhumiwa inatosha
kusimamishwa na kupisha uchunguzi.
Mwisho polisi wetu ni wanausalama wetu, polisi
wananyanyasa si kwamba wanapenda.
Tuliandika tume ya utumishi ya jeshi la polisi,
tulipendekeza ili mambo ya yao na ajira zao
ziwe safi lakini wamefuta.
Mkuu wa Jeshi la polisi afanye kazi kwa weledi,
Jeshi la polisi lizingatie kiwango cha taaluma,
haki zabinaadamu, uwazi na uwajibikajikaji,
mahusiano na jamii lakini yote wamefuta.
Tume ya uhusiano na uratibu ili kuondoa
migongano ya muungano kikatiba, bahati mbaya
imefutwa.
Tuendelee kujadiliana badala ya kuwaachia
viongozi wakajifungie peke yao.
MWESIGA BAREGU
Asante sana, Polepole alipomalizia nataka
nianzie, vijana mmenifurahisha mlivyojaa.
Mmoja wa wajuu zangu nilipoteuliwa kwenye
tume, aliniagiza kila mtu asomeshwe mpaka
darasa la 12, tukaliweka usigombee ubunge
mpaka ufike darasa la 12 lakini wameliondoa.
Maridhiano, tulipitia wakati mgumu sana chini
ya mwenyekiti kujenga mahusiano. Njia ya
maridhiano na kuelewana kufikia maafikiano.
LIKE Ukurasa wetu MJUMBE BLOG facebbook au Tutembelee mtandaoni kea kuandika MJUMBE BLOG kisha ingia hapo upate picha,Matangazo,habari mpya,Matukio muhimu kila mara.
©Mjumbe Blog Volunteers
Post a Comment