PENGO AJITOKEZA:"NIOMBEENI;AFYA YANGU INA IMARIKA"!
"Namshukuru Mwenyezi Mungu, lakini pia
nawashukuruni nyote kwa sala zenu na dua zenu
zilizoniwezesha hata kusimama hapa mbele yenu
saa hizi kama mnavyoniona," alisema huku
akishangiliwa na mamia ya waumini wa kanisa
hilo.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar
es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
amesema kuwa hali ya afya yake inaendelea
kuimarika. na kuwataka waumini kuendelea
kumwombea.
Akizungumza kwenye Misa Takatifu ya Mavuno na
shukurani kwa jimbo hilo, iliyofanyika jana
Msimbazi Center jijini Dar es Salaam, Pengo
alisema ameamua kuitumia siku hiyo kumshukuru
Mungu kwa kuwa ndiye alimfanya kuwa hai hadi
sasa.
"Namshukuru Mwenyezi Mungu, lakini pia
nawashukuruni nyote kwa sala zenu na dua zenu
zilizoniwezesha hata kusimama hapa mbele yenu
saa hizi kama mnavyoniona," alisema huku
akishangiliwa na mamia ya waumini wa kanisa
hilo.
Alitumia muda huo kuwaasa waumini kuwa na
tabia ya kushukuru kutoka ndani ya mioyo yao,
akisema ndilo jambo linalompendeza Mungu.
LIKE page yetu MJUMBE BLOG au Tutembelee Mtandaoni andika MJUMBE BLOG uingie hapo kwa picha,matangazo,Taarifa mpya,Habari muhimu kila mara.
©Mjumbe Blog Vo
Post a Comment