
Mnenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta na Extra
Bongo, Aisha Madinda amefariki dunia leo.
Taarifa kuhusu kifo chake kimedai kuwa
mnenguaji huyo mahiri amefariki kwenye hospitali
ya Mwananyamala. Zingine zinadai alifikishwa
katika hospitali akiwa ameaga dunia tayari.
Bado haijafahamika alikuwa akisumbuliwa na
ugonjwa gani. Taarifa zaidi zitakujia baadaye.
SOMA TAARIFA ZAIDI HAPA.....
Aisha Madinda wakati wa Uhai wake
Aliyekuwa Mnenguaji na Muimbaji wa
Bandi ya Twanga Pepeta Aisha
Madinda amefariki dunia hivi punde
Jijini Dar es salaam.
Habari
imethibitishwa na mmiliki wa bendi
ya Twanga pepeta Asha Baraka.
Mkurugenzi wa bendi ya Twanga
Pepeta amesema kuwa alipewa taarifa
na Daktari mmoja kuwa wameona kama
mwili wa Aisha Madinda hospitalini
hapo, ndipo akatuma watu kwenda
kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili
kuhakikisha kama kweli ni yeye
ndipo walipogundua ni yeye.
“ Mimi nipo njiani natoka Kigoma
kuja Dar es Salaam, ni habari ya
kusikitisha sana maana Aisha
amefariki katika mazingira ya
kutatanisha sana, jana alikuwa
mzima na anachati na watu kwenye
simu leo napigiwa simu mwili wake
umekutwa umehifadhiwa kwenye
hospitali ya Mwananyamala, hata
sielewi nini kimetokea”.
Amesema
Asha Baraka
Mungu ailaze roho ya Marehemu Aisha
Madinda mahali pema peponi.
©Mjumbe Blog Volunteers
posted from Bloggeroid
Post a Comment