Unknown Unknown Author
Title: BUSTANI YETU IME VUNWA YOTE:KWA KHERI FOREST YA MLOWO! KWA KHERI LOVE GARDENI YETU...!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kama ukitembelea Kijiji cha Mlowo kinacho kua kwa kasi ya Uyoga(Mushroom rate),Ni nadra sana kukutana na msitu wa miti iliyo pandwa kwa usta...
Kama ukitembelea Kijiji cha Mlowo kinacho kua kwa kasi ya Uyoga(Mushroom rate),Ni nadra sana kukutana na msitu wa miti iliyo pandwa kwa ustadi na kitaalamu kama ukiondoa eneo linalo julikana kama FOREST huko ndiko eneo pekee ambalo unge weza kushuhudia ekari kama Tano au Nane zikiwa zime pandwa miti.Sehemu ambayo ili aminika kuna utulivu wa kutosha unapo kuwa kijijini MLOWO,kwani una kuwa mbali na kelele za kutwa za katikati ya kijiji hicho,mbali na watu,Mbali na barabara kuu ya Dar-Tunduma,Mbali na Viwanda mbalimbali ila una jikaribisha na Ukijani ulio chipiua na kupendeza macho kwa uasili na milio ya ndege pori kwa wingi. Utamaduni ambao kwa jamii huska hauku dumishwa,Pamoja na faida za upandaji wa miti katika mazingira na maisha ya mwanadamu kwa ujumla;Kamera ya MJUMBE BLOG jana imeshuhudia Msitu ule wote ukiwa ume vunwa,Shuhudia mwenyewe kwa kufuatilia picha hapa:- Pichani ni milingoti ya shamba la bustani ya Mlowo ikiwa ime katwa yote na kuanza kupasuliwa mbao Sehemu ya shamba ikiwa ime katwa miti yote na kuiacha miti ya asili tu michache ambayo ilikuwepo eneo hilo Hii ndiyo Taswira utakayo kutana nayo kama ukitembelea ulio kuwa mstitu wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi,Katika kijiji cha Mlowo(Forest) Hali ilivyo sasa ni uangavu unao kuwezesha kufikia kuona kata upeo wa macho yako hakuna msitu tena hakuna ule ukijani wenye giza tena ambao ulibuniwa kama kivutio kwa vijana wengi ndani ya kijiji cha Mlowo. Pichani ni Mdau Mwenza wa MJUMBE BLOG akiwa eneo la Tukio ambapo alishuhudia magari yanayo beba mbao kutoka katika bustani hiyo,Akina mama na watoto wakijibebea kuni na mabanzi pia Picha Zifuatazo Zilipigwa mwaka juzi zikionesha sehemu ya Bustani hiyo ambayo ilijulikana kama FOREST Sehemu ya Msitu huo kama ulivyo kuwa ukionekana pichani mwaka juzi,(Picha na Maktaba)

posted from Bloggeroid

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top