Unknown Unknown Author
Title: KIFO CHA AISHA MADINDA:HIKI HAPA NDICHO AME KIONGEA MTOTO WAKE!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Pichani ni Aisha Madinda enzi za uhai wake Stori:waandishi wetu MENGINE yameibuka! Kifo cha aliyekuwa mnenguaji wa Bendi ya The Afr...
Pichani ni Aisha Madinda enzi za uhai wake






Stori:waandishi wetu MENGINE yameibuka! Kifo cha aliyekuwa mnenguaji wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ kimeibua mengine ambapo baadhi ya watu wa karibu wanaamini kimetokana na kudungwa sindano tano za majimaji yenye madawa ya kulevya, ‘unga’ na rafiki yake, Ijumaa ‘Kubwa’ linakupa zaidi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Aisha alidungwa kwa makusudi sindano hizo na rafiki yake mmoja ambaye polisi bado wanamtafuta, ikidaiwa lengo lilikuwa kummaliza.
YALIYOSEMWA
Akizungumza kwenye msiba wa mnenguaji huyo nyota nyumbani kulikokuwa na kilio, Kigamboni jijini Dar, mwombolezaji mmoja ambaye ni mtu wa karibu na marehemu alisema:
“Unajua siku za karibuni, Aisha alirudia kubwia unga kama zamani, sasa majuzi mimi nilikutana naye akasema yuko kwa rafiki yake, Mwananyamala (Dar), lakini huyo rafiki aliyenitajia ni mmbwia unga mkubwa na amekuwa akiwadunga sindano wenzake.


Mtoto wa marehemu Aisha, Naomi akiwa katika majonzi.
“Sasa si unajua kwamba, sindano zile ukidungwa bila kipimo ni sumu mwilini. Uwezekano ni mkubwa kwamba, sindano alizodungwa na mwenzake ndizo zimechukua uhai wake,” kilidai chanzo hicho.
CHANZO KINGINE
Kwa mujibu wa chanzo kingine msibani hapo, upo wasiwasi kwamba tangu Aisha arejee Bongo akitokea Dubai kuna mtu amekuwa akimtishia maisha kwamba atamtoa roho.
Chanzo hicho kilidai kwamba, staa huyo ambaye alirudi akiwa vizuri amekuwa akipewa vitisho na mtu huyo bila kutaja sababu.
SIKU YA KIFO
Siku ya tukio, juzi Jumatano, habari zinadai kwamba, Mkurugenzi wa Vipindi wa Radio Clouds FM, Ruge Mutahaba alipigiwa simu na daktari mmoja wa Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Kinondoni, Mwananyamala na kuambiwa kuwa, kuna mwili wa mtu anayefanana na Aisha Madinda umetelekezwa hospitalini hapo na watu wasiojulikana na wameondoka.
Baada ya taarifa hizo, Ruge alimwendea hewani Bosi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka na kumjulisha madai ya daktari.

Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’Asha Baraka.
“Asha Baraka alikuwa Kigoma. Kwa hiyo alipopewa taarifa hizo alimpigia simu kiongozi wa wanamuziki wa Twanga Pepeta, Luiza Nyoni Mbutu na kumpa maelekezo kwamba afuatilie habari alizoambiwa na Ruge kama ni kweli.”


AISHA MADINDA NDANI YA MOCHWARI
Ikazidi kudaiwa kuwa, Luiza na wanamuziki wenzake, Lilian Tungaraza ‘Lilian Intaneti’ na Maria Soloma walifunga safari hadi Mwananyamala na kuukuta mwili wa Aisha ukiwa tayari mochwari, wakamjulisha Asha ambaye alifunga safari na machozi juu kurejea Dar.

MTOTO WA MAREHEMU, ANAITWA NAOMI
Akizungumza na gazeti hili ndani ya Hospitali ya Mwananyamala muda mfupi baada ya mwili wa mama yake kuingizwa mochwari, binti wa Aisha, Naomi huku akimwaga machozi, alisema:
“Mama alikuwa akiishi Kigamboni siku za karibuni. Mimi pia nikaamua kwenda kuishi naye.”
Akaendelea: “Kuna kama siku tatu nyuma mama hakuwa akilala nyumbani, jana (Jumanne sasa), asubuhi mama alinitumia meseji akisema anaomba nimtumie pesa, nikamtumia.
“Lakini leo (juzi, Jumatano) mchanamchana nilisema nimpigie simu mama nimuulize huko aliko anaendeleaje? Kabla sijafanya hivyo, mama mkubwa alinitumia meseji na kuniambia mama amefariki dunia, ndiyo nikaja huku.”

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere 'Steve Nyerere' (kulia) na Luiza Mbutu (katikati) wakihesabu michango iliyopokelewa kwa njia ya simu katika Hospitali ya Mwanayamala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mnenguaji wa kitambo, Lilian Intanet.
KIKAO CHA FAMILIA AELEZEA KIFO CHAKE!
Binti huyo aliendelea kusema kuwa, siku za karibu, marehemu aliwahi kuwaita ndugu zake na kuwapa ujumbe wa ajabu.
“Kuna siku aliwaita ndugu zake nyumbani akasema katika familia yetu wote, mimi ndiyo nitakayeanza kufa. Sijui mama alijua atakufa ndiyo maana akasema vile,” alisema binti huyo.
MASWALI YA MSINGI
Mpaka sasa maswali ambayo yalitawala msibani ni haya! Je, ni nani aliyeufikisha mwili wa marehemu Hospitali ya Mwananyamala na kuutelekeza? Je, dokta alijuaje kuwa alikuwa Aisha Madinda?
Je, mwili wake ulipelekwa hospitalini hapo na mtu mmoja au wengi? Walitumia usafiri gani? Bajaj au teksi? Ni vyema pia polisi wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar wakafuatilia kifo hiki kwa undani. Inna lillah, wainna ilaih rajiuu

SOMA ZAIDI WASIFU WAKE HAPA

Aisha Madinda akiwa na mkurugenzi wa ASET Asha Baraka.
Makala: Sifael Paul na Gladness Mallya
Amekwenda mapema mno! Siku ya Desemba 17, mwaka huu haikuwa poa hata kidogo kwenye tasnia ya muziki wa dansi Bongo katika kipengele cha unenguaji.
Chumba chetu cha habari cha Global Publishers kinachofanya kazi kwa karibu na mastaa Bongo kilipata mshtuko wa aina yake.
Zilikuwa ni habari mbaya za kifo cha aliyekuwa mnenguaji bei mbaya wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ inayosimamiwa na Kampuni ya ASET chini ya mkurugenzi wake, Asha Baraka, Mwanaisha Mohamed Mbegu. Wengi tulimzoea kwa jina la stejini la Aisha Madinda.
AZALIWA OCEAN ROAD
Katika mahojiano aliyofanya na magazeti yetu kwa nyakati tofauti, kabla ya kujiingiza kwenye sanaa ya unenguaji na baada ya kuugua kwa muda mrefu kisha kupona na kukutwa na umauti, Aisha alieleza kwamba alizaliwa jijini Dar katika Hospitali ya Ocean Road.
KIGOMA
Hiyo ilikuwa Mei 5, 1979. Hivyo ameondoka mapema akiwa na umri wa miaka 35 tu. Baada ya maisha ya utoto, Aisha alipelekwa mkoani Kigoma ambako ndiko alikokulia.
Akiwa mkoani humo, Aisha alipata masomo yake ya msingi katika Shule ya Kiganamo iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi alipohitimu darasa la saba mwaka 1992.
AISHIA FORM TWO
Mwaka 1993 alihamishia makazi yake mjini Kigoma na kujiunga na Sekondari ya Katubuka. Hata hivyo, Aisha hakufanikiwa kuhitimu masomo yake ya sekondari baada ya wazazi wake kushindwa kumlipia ada hivyo aliishia kidato cha pili (form two).
DAR
Mwaka 1994, Aisha alihamia jijini Dar na kuanza kazi ya usafi katika kampuni iliyojulikana kama Dar Cleaner. Alifanya kazi hiyo katika majengo mbalimbali ya jijini hivyo kufahamiana na watu wengi.
UNENGUAJI
Mwaka 1996 aliingia kwenye unenguaji baada ya prodyuza wa muziki aliyefahamika kwa jina moja la Maloni kumtonya kuwa Club Bilicanas ‘Bilz’ iliyopo Posta, Dar kulikuwa kunahitajika wanenguaji.
Akiwa Bilz, mwaka huohuo, klabu hiyo ilianzisha bendi iliyokwenda kwa jina la Bil Bams ndipo Aisha akaanza kuitumikia.
UARABUNI
Mwaka 1999, wakati huo, Aisha alishakuwa tishio katika kukata nyonga stejini huku akieleza jinsi alivyoipenda kazi yake hiyo.
Mwaka huohuo, alipata shavu la kwenda kupiga kazi Uarabuni katika Mji wa Muscat akiwa ameambatana na mcheza shoo mwenzake, Halima White ambaye sasa ni marehemu.
Walikaa nchini humo kwa takriban mwaka mmoja, mwaka 2000 walirejea Bongo wakiwa mambo safi.
BORABORA SOUND
Mwaka huo Aisha alijiunga na Bendi ya Borabora Sound ambayo aliitumikia kwa miezi sita kabla ya kusafiri tena kwenda Bahrain, Uarabuni kwa kazi hiyo ya unenguaji.
KILIMANJARO CONNECTION
Baadaye Aisha alirejea Dar kwa mara nyingine. Alijiunga na Bendi ya Kilimanjaro Connection ya jijini Dar ambapo pia hakukaa sana.
Mwaka 2000 mwishoni, aliachana na bendi hiyo kisha akawa anafanya biashara zake ndogondogo.
Aisha Madinda.
TWANGA PEPETA
Mwaka 2001, mkali huyo wa kukata nyonga anayeshikilia rekodi hiyo kwa kipindi chote alijiunga na Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’.
UHOLANZI
Aisha alifanya safari nyingi za kisanaa barani Ulaya akiwa na Twanga Pepeta lakini hawezi kusahau shoo aliyokwenda kufanya nchini Uholanzi katika Mji wa Amsterdam ambako alipokelewa kwa shangwe ya ajabu kiasi kwamba hakuamini macho yake.
EXTRA BONGO
Hapo alipiga kazi ya unenguaji hadi mwaka 2011 mwishoni alipohamia Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo Staili’.
Kwa bahati mbaya, wakati huo Aisha tayari alikuwa ameshatopea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya hadi kufikia hatua ya kushindwa kunengua akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu. Hata hivyo, alitangaza kuacha kutumia madawa hayo japokuwa baadaye kuliibuka ‘rumansi’ kuwa bado alikuwa akitumia.
REJEA TWANGA
Mwaka jana, mwanamama huyo alirejea Twanga Pepeta lakini bado alikuwa akisumbuliwa na miguu huku akitumia dozi ya kuacha madawa ya kulevya na kuhamasisha vijana kuacha ulevi huo mbaya unaomaliza nguvu ya taifa ambayo ni vijana.
OKOKA
Katika kutafuta msaada wa kiroho, Aisha aliokoka akawa anasali katika Kanisa la Zoe lililopo Segerea jijini Dar akiyakabidhi maisha yake kwa Mwenyezi Mungu hadi alipokutwa na umauti.
DUBAI
Hata hivyo, miezi kadhaa mwaka huu, mwanadada huyo alitimkia Dubai kwa ajili ya dili la kunengua lakini alipofika huko alijikuta akitumikishwa kazi za ndani na wenyeji wake kiasi cha ubalozi wa Tanzania huko Dubai kuingilia kati na kumrejesha nyumbani.
MAFANIKIO
Aisha, mara zote alikuwa akitoa shukrani za pekee kwa uongozi wa Twanga Pepeta kwani kipindi anaitumikia, alifanikiwa kumiliki nyumba, viwanja na gari.
KIFO
Siku moja kabla ya kifo, Aisha alikuwa akichati na marafiki zake ambao kwa pamoja walishindwa kuamini kusikia amefariki dunia. Mnenguaji huyo ambaye alijituma kujiajiri na kuwa mfano wa wanawake watafutaji, alitarajiwa kuzikwa jana nyumbani kwake Kigamboni, Dar.
WATOTO
Kwenye maisha yake ya unenguaji, Aisha amefanikiwa kupata watoto wawili kwa baba tofauti, Feisal na Naomi.
Rest In Peace Aisha Madinda. Amen!

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top