BREAKING NewZ:MAJANGA PICHANI:MZIMU WA AJALI BADO UNAZITAFUTA ROHO ZA WASAFIRI MBOZI!!
Mzimu wa ajali bado ume endelea kutafuta roho za wasafiri wilayani Mbozi,Mbeya! Ni mishale ya saa nane mchana na madakika eneo la Vwawa,Mbimba Pale lori lililo kuwa lime sheheni tani kadhaa za mahindi lilipo gongana na gari dogo la IT lililo kuwa likitokea bandarini huku madereva wote wawili wakiwa kwenye mwendo na kusababisha kupasuka kwa tairi la mbele la dereva la roli na mwenye gari ndogo kubetuliwa,hivyo kusababisha mwenye gari kubwa baada ya kugongana kukosa uelekeo na kuanguka mita chache tu mbele barabarani na kusababisha foleni ya magari kwenye barabara kuu Dar-Tunduma.Katika ajali hiyo hakuna aliye poteza maisha,ziadi ya uharibifu wa vyombo vya moto(gari dogo na Lori).Mashuhuda wa ajali hiyo wame wame sema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo kupoteza uelekeo kwa sababu ya uchovu,hivyo kupitiwa na usingizi na alipo shituka alikuwa amesha kutana na Lori hilo!
Pichani ni mwonekamo wa gari ndogo aina ya (IT) ikiwa imesha haribika upande wa dereva,baada ya kupata ajali eneo la Mbimba;Vwawa
Pichani ni lori lililo gongwa na gari ndogo likiwa lime anguka baada ya kupasua Tairi eneo la Mbimba Vwawa
Pichani ni foleni iliyo sababishwa na ajali husika mara baada ya kuziba njia kuu ambayo ni barabara ya Dar-Tunduma hivi punde
********************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************
Picha Na Mdau mwenza wa MJUMBE BLOG aliye kuwa eneo la tukio








Post a Comment