MTI WA DAWA.....!
Ni jambo la Kawaida kwa watu waishio kijijini kupendelea kutumia miti shamba kwa ajili ya matibabu ya maradhi yawasumbuayo,haijalishi ni kwa maradhi ya msimu ama yale ya mlipuko.
Na hata kijijini kuna wazee wa vijiji hivyo ambao kwa kutumia uzoefu wao wame jijengea heshima za kitababu kiasi kwamba kuna wanakijiji,ambao hawa amini kuwa zahanati ni mahali salama zaidi kwa wao kupewa huduma za kitabibu.Wazee wengi katika hao ni watalaamu wa miti shamba! Wanatumia uzoefu wao katika elimu ya mimea kuihudumia jamii yao.Ukipita mbugani ni rahisi kukutana na miti ambayo ime chimbwa dawa.... Lakini kujua mti huo ni dawa gani ni Jambo jingine! Mti uchimbwao dawa haukatwi! huachwa uendelee kukua kwa manufaa ya kizazi kijacho. Elimu hii wanayo wachache na huirithisha kwa kizazi chao kwa siri nzito! Kwahiyo Usije ukafunga Safari kwenda kwa kila mzee anaye ishi kijijini uka amini ataijua vema miti shamba! Wengine ni wazee wa Makanisa tu... achana na wale ambao ni wazee wa benchi la ufundi katika ligi za Mbuzi huko vijijini....
Post a Comment