PICHA ZAIDI YA KUMI ZIARA YA KUWA ONA WATOTO YATIMA MBOZI MISION YAFANIKIWA TENA!! TAZAMA ILIVYO KUWA HAPA!!
Wapendwa....
Nashindwa nianzie wapi kusema haya niliyoyapanga kuyasema...I am speechless!!!
Daaaah....
Namshukuru saana Mungu kwa ukuu wake kwa kutupa pumzi hadi sasa..hakika hatuna cha kumrudishia..sifa na utukufu ni vyake Mungu.
Mungu amelisimamia hili na limefanikiwa..asante sana Mungu!!
Ni washukuru kwa dhati kabisaa ndg zangu waliojitoa kwa michango yao ya kifedha,vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto wetu...ni washukuru kwa dhati pia wale wote waliokuwa nasi kwa maombi kwani mara nyingi hupenda kuharibu mipango mizuri ya kimungu..mbarikiwe saana kwa hili wapendwa...
Niwatie moyo pia wale ambao kwa namna moja au nyingine walitaka kuchangia lakini walikwama kwa sababu mbalimbali
Mungu atawafanyia wepesi safari nyingine nanyi mtajumuika nasi vile mtakavyoguswa wapendwa...
Msife moyo kwani bado tuna nafasi nyingine nyingi tu za kwenda kuwafariji watoto yatima kama Mungu akiendelea kutupa uzima!!
Mungu ni mwema saana tumeweza kufanikisha hili zoezi kwa mwaka wa pili mfululizo tena kwa mafanikio makubwa sanaa ..
Hatupaswi kujisifu kwani si kwa uwezo wetu ila ni kwa mapenzi yake yeye!!
Niwashukuru wote waliojitoa kwa ajili ya kuungana nasi kwajili ya ziara yetu..mmeacha shughuli zenu na kutenga muda kwa ajili ya hili ili lifanikiwe..barikiweni saana sanaa!!
Muendelee na moyo huo huo!!
Kwa mlioshindwa kuungana nasi kwa sababu mbalimbali msisononeke naamini wakati mwingine Mungu atawapa kibali mtalitekeleza hili..zaidi niwahakikishie kuwa tuliwawakilisha vizuri saaaana!!
Safari yetu ilianza saa tisa alasiri kuelekea Mbozi mission safari ilijumuisha wajumbe wapatao sita..
Silla Aron Yalonde Wumbura Mwashiozya
Amius Mwala
Elastic Mbellah
Fasihi ya Wanyiha(Michael Mwampashe)
Eddy Shonza na
Missana
Ujumbe uliwasili saa 9:30 alasiri na kupokelewa na wenyeji wetu waliokuwa watatu!!
Ujumbe wetu ulibeba zawadi zifuatazo kwajili ya watoto yatima
1.SUKARI KATONI MOJA (1)NA KILO TISA
2.SABUNI ZA MCHE KATONI 2
3.SABUNI ZA UNGA NDOO KUBWA TATU
4.SABUNI ZA KUOGEA DAZANI NNE (4)
5.PIPI DAZANI MBILI (2)
6.MAFUTA YA KULA NDOO NDOGO MOJA(1)
7.PAMPERS KUBWA DAZANI TATU(3)
8.MAFUTA KUPAKAA DAZANI MBILI(2)
9.KARANGA DEBE
10.ULEZI DEBE
11.MAHINDI DEBE
12.SOYA DEBE
13.MCHELE DEBE
14.UNGA WA LISHE KILO 8
15.NYAMA KILO 5
16.NGUO AINA MBALIMBALI(MASWETA,SURUALI,FULANA,KOFIA ZA BARIDI,MASHATI,VIGAUNI NK)
17.PESA TASLIMU 30000/=
Vitu vilivyonunuliwa vilizingatia mahitaji halisi ya kituo hiki...
Mratibu alitukaribisha na akatoa historia fupi ya kituo..
Changamoto na mahitaji ya kituo..zaidi akatuelezea kuhusu ufadhili wa kituo kuwa upo chini ya Kanisa la Moraviani jimbo la kusini Magharibi..lakini pia wadau na wahisani mbalimbali..watu binafsi..taasisi na vikundi mbalimbali Wanyiha wa Mbozi na Marafiki tukiwamo..alitoa shukurani nyingi kwetu kwa moyo wetu wa kujitoa kwaajili ya watoto yatima!!
Akasema hana maneno sahihi ya kutuambia zaidi ya kusema Mungu atuzidishie pale tulipotoa...akasema asante sanaa saanaa!!
Admini wa group alisimama na kutoa historia fupi ya kundi letu malengo na dira yake...
Akatoa shukurani za dhati kwa wenyeji wetu kwa moyo wao mkuu wa kuwalea watoto wale katika mazingira halisi tuliyoyaona yenye changamoto nyingi saana...akawasihi wazidi kujitoa kwajili ya hili na Mungu atawalipa kwa wanachokifanya..
Alitoa shukurani kwa wanakikundi kwa moyo wao na mshikamano wao mkubwa hadi leo...
Picha za ukumbusho zilipigwa na wanakikundi walifurahi kwa kuchezacheza na watoto wetu...
Baada ya hapo tuliaga saa 11:00 jioni na kuelekea Vwawa..ambapo kilifanyika kikao kidogo cha tathmini na saa 12:30 tulitawanyika..
Naomba niwataje kwa majina ndg zetu waliofanikisha zoezi hili moja kwa moja
1.Eddy Shonza
2.Tumaini Mwamundi
3.Wanseho Simbeye
4.Edson Mwashiozya
5.Alfan Andekisye(Dickens Stephen Zero)
6.Happy Nzunda
7.Amassa Mwasubila
8.Hawa Julius
9.Grace Kapekele
10.Neema Mwashambwa
11.Angolwisye Ngaluma
12.Ernest Messa
13.James Wumbura
14.Abraham Mwampashe
15.Atu Mwamakula
16.Pendo Simbaliana
17.Mai Sala
18.Lily
19.Muddy
20.Rahel Shega
21.Rahim Mwashilindi
22.Mwanda Alpheous
23.Amina Mwashambwa
25.Mbushi Mwashambwa
26.Rehema Kalonge Benard
27.Annie Tunduma
28.Anna Dar es salaam
29.Salum Jerry
30.Hamis Nzunda(Mwalimu Nzunda)
31.Bernard Wumbura
32.Aliko Lyela
33.Tatu Nzowa
34.Yolamu Gwaya
35.Suma Sykilili
36.Michael Mnkondya
37.Wilson Kalambo
38.Emmanuel Msanganzila
39.Elastic Mbella(Mjumbe blog)
40.Michael Mwampashe
41.Nicter Shitindi
42.Ernest Mswima
43.Nsalu Ngaikwela Nzowa
44.Joseph Mgale
45.Jacob Mwashiozya
46.Stella Sawala
47.Veronica Hamisi Mwambwalo
48.Emmanuel Nzunda(Mbomboyoka)
49.Albert Chenza
50.Grace Sinkamba Minja
51.Lydia Masawe(Manka)
52.Gabriel Misana
Barikiweni saana!!!
Mungu awazidishie pale mlipopunguza...
Mwisho kabisaa niwaombe radhi wale wote niliowakwaza kwa namna moja au nyingine wakati natimiza majukumu yangu ya kukumbusha mchango kwa kuwapigia simu na mameseji kibaoo tusameheane mweeee...
Ila yote kwa yote mission accomplished!!!
Barikiweni mnoooooo!!!
*********************************************************************************************************************************
Taarifa Imetolewa na Mratibu wa Safari ndugu Silla Yalond Wumbura Mwashiwozya
Nawatakia mafanikio ktk kazi za mikono yenu...
Amen.
_________________________________________________________________________________________________________________________________Historia Fupi ya Kituo cha yatima Mbozi mision kama ilivyo tolewa na Msimamizi mkuu Bi Rehema Mwapule!
Bi Rehema alisema 'Aliye toa wazo la tunacho kiona leo hapa ni Bi Elizabeth,Alikuwa ni mwenye asili ya Uswisi Alifika Tanzania mwaka 1947,alikuja kwa ajili ya shughuli za ukunga! Lakini katika kazi yake hiyo alikumbana na Changamoto ya Kuona baadhi ya akina mama walio kuja kupata huduma wakipoteza maisha ya na kuwa acha watoto wachanga bila malezi yao.Ilipotokea kwa mara ya kwanza aliamua kumuchukua mtoto huyo mmoja ili ampe malezi kama mzazi.Aliendelea hata walipo fikia wanne,na hapo ndipo aliona ni vema kama kuta kuwa na Chumba maalum kwa ajili ya watoto hao hasa walio fiwa na mama.Katika kutoa huduma yake hiyo y ukunga baadaye alipata wazo la kujenga hospital itakayo kuwa ina toa huduma kwa watu wote ndani ya jamii,na huo ukawa mwanzo wa Hospitali ya Mbozi mision Tunayo iona leo.
Pichani ni Mratibu wa Ziara akiwakabidhi walezi wa watoto Yatima katika kituo cha Mbozi mision,Jana Jioni
_________________________________________________________________________________________________________________________________
Ingawa awali wazo lake Bi Elizaberthi Lilikuwa ni kuwa na kituo kwa ajili ya watoto walio fiwa na mama tu mwaka 1976 aliokotwa mtoto asiye julikana ni wa nani,Ndipo alipo Badili wazo la kuanza kuwa lea watoto wote wasio na wazazi na wale walio Okotwa wakiwa wametelekezwa majalalani,Njiani na Wengine kutupwa porini na kuokotwa na wasmaria wema.
Baadhi ya wawakilishi wakiwa wame wasiri eneo la kukutana ambapo ilipangwa iwe katika Mji wa Vwawa,Mbozi(CHAMPION HOTEL)
_________________________________________________________________________________________________________________________________
Akaona ni vema kama hao watoto watapatiwa uangalizi maalum,mpaka watakapo kuwa na uwezo wa kula Chakula kama ana mzazi wa kiume alikabidhiwa kwa taratibu za kisheria kama mzazi ili amlee mwenyewe.Lakini kwa wale ambao wazazi wao wana kuwa hawajulikani basi huwa Wana endelea kwa kuwa lea mpaka watakapo fikia umri wa kwenda Shule na wakisha Timiza Umri wa miaka kama Kumi na mbili mpaka kumi na Tatu Wakiwa tiari wamesha maliza Shule ya msingi huwa wana pelekwa Kurasini,Dar es Salaam ambacho ni kituo cha kupokea watoto wenye umri huo mpaka watakapo timiza Miaka kumi na nane ambapo hupelekwa mafunzoni ili wapate Elimu ya Kujitegemea na kuwa watu wenye tija kwa Taifa tena.
Pichani ni sehemu ya wawakilishi waki anza safari kuelekea Mbozi Mision,Kilipo kituo cha kulelea watoto yatima,mida ya saa tisa arasiri jana
_________________________________________________________________________________________________________________________________
Kituo ni mali ya kanisa moravian lakini hakichagui mtoto wa kumpokea kwa misingi ya Dini wala imani yoyote.Mtoto mwenye vigezo vya kupokelewa kituoni hapo hupokelewa na kulelewa.Na Utaratibu wa kumpokea mtoto hapa lazima apitie ngazi zote kuanzia ngazi ya Barozi wa nyumba kumi,Mwenyekiti wa kitongoji mpaka Ofisi ya Mtendaji ijiridhishe na ibariki kwa maandishi ndipo mtoto Hupokewa kwa misingi ile ile na Mawasiriano kati wa kituo na Mtendaji huendelea.
Baada ya maelezo kutoka kwa Bi Rehema,ali Ruhusu maswali na majadiliano kama kuna mahali hakueleweka ili abainishe vema.
Moja ya picha ya Kumbukumbu iliyo pigwa eneo la kuondokea kuelekea sehemu walipo watoto hao,Katika mji Vwawa
_________________________________________________________________________________________________________________________________
Safari ya kuelekea eneo la tukio ikiwa ina endelea,sehemu ya wawakirishi wakiwa ndani ya Usafiri wao
Picha ya kumbukumbu sehemu ya wawakirishi walipo wasiri eneo la tukio,Mbozi mision wanapo lelewa watoto Yatima hao jana jioni,
Pichani wawakirishi walivyo pokewa na walezi wanao wahudumia watoto yatima kituo cha Mbozi mision
Pichani ni eneo lililo andaliwa maalum kwa ajili ya wawakirishi wa Ziara ya kuwa tembelea na kuwa ona yatima Mbozi
Pichani ni Watoto husika wakiwa Mikononi mwa walezi wao na wengine wakiwa wame kaa chini kama wanavyo onekana katika picha mbili hapo juu
Pichani ni Mratibu wa Safari aki toa utambulisho na maelezo kwa ufupi ya dhima ya safari husika na kuwa taja wadau mbalimbali walio wezesha zoezi hili kukamilika na kusema alio waona ni kama wawakirishi wa wengi ambao hawakuweza kufika kutokana na majukumu mbali mbali na maeneo waliyo kwa sasa.
Kuna mdau ali kaririwa akisema kuwa eti huyu mtoto pichani juu ame fanana na aliye mbeba... kwahiyo aka acha usemi kuwa ina wezekana ni ndugu mtu!!
Mratibu wa Safari aki agana na walezi wa watoto yatima
Naam;Wasikuambie wao ni akina nani?? Yatatzame Matendo yao Utawajua!!
*********************************************************************************************************************************Picha Zote na MAELEZO Na mdau wa MJUMBE BLOG
_________________________________________________________________________________________________________________________________
Post a Comment