Unknown Unknown Author
Title: SOMA HAPA WALICHO ANDIKA AKINA ZITTO,KAFULILA,EDDO,SHIGONGO,R.O.M.A;BAADA YA HOTUBA YA RAIS KWA WAZEE WA DAR LEO JIONI!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
. Alicho Post; Julius Mtatiro TATHIMINI YANGU KUHUSU HOTUBA YA RAIS KIKWETE YA LEO, HASA KATIKA WIZI WA FEDHA ZA TEGETA ...


.

Alicho Post;
Julius Mtatiro


TATHIMINI YANGU KUHUSU HOTUBA YA RAIS KIKWETE YA LEO, HASA KATIKA WIZI WA FEDHA ZA TEGETA ESCROW.
1. Nilitarajia angezungukazunguka ili kujaribu kuokoa mwizi huyu au yule - Imekuwa hivyo.
2. Kwa kiasi kikubwa maazimio ya bunge ameyakwepa kwepa tu, ilimradi asiyatekeleze kabisa au akitekeleza iwe hivyo nje ya wakati.
3. Rais ameshindwa kuongea kama mkuu wa nchi, kuwaonesha watendaji na washirika waje kuwa anachukia rushwa, haitaki na anaipiga vita. Kila aliyehusika na wizi wa fedha hizi au mgao wake, rais hasemi kwa uwazi kuwa amevunja taratibu za uongozi, anazungukazunguka.
4. Bodi ya TANESCO ilipaswa kufukuzwa kazi, si kuacha ati imalizie muda wake kwa sababu uko ukingoni. Mchezo huu ni kama ule wa EPA, badala ya kuwaadhibu wezi na kuwaondoa madarakani , wanaombwa warudishe fedha tu.
5. Rais anaonekana hajui msingi wa uchunguzi wa ripoti ya CAG na majumuisho ya PAC. Au amepotosha kila kitu kimakusudi, anahitaji uchunguzi mpya kuchunguza nini ambacho vyombo vya serikali na bunge havijachunguza?
6. Inaonesha wazi kuwa, rais hayuko tayari kuona washirika wake walioiba fedha au kunufaika nazo, wakifikishwa mahakamani.
7. Amejaribu kuonesha ati kashfa hii walioshughulikia ni CCM, na kwamba kama wangeamua kuiacha isingefika hapa ilipo. Rais anasahau kuwa kashfa hii iliibuliwa na gazeti ka THE CITZEN na mbunge DAVID KAFULILA (NCCR) na kusimamiwa kidete na wabunge wa upinzani, na kwamba wabunge wa CCM walikuwa mbogo baada ya kuona watanzania wamekasirika.
8. Inaonesha kuna mgawanyiko mkubwa sana serikalini, na mambo mengi ambayo Rais kayasema leo yalikywa hayajaamuliwa vizuri, ni kama washauri wake walimuachia yeye mwenyewe amalizie, maana waliona watajikaanga kujaribu kukwepa maazimio ya bunge ambayo yako wazi na yalifikiwa baada ya uchunguzi mkubwa.
9. Kikwete ataondoka madarakani huku 9|10 ya maazimio ya bunge hayajatekelezwa.
10. Viongozi wa CCM, Kinana na wenzake, watakuwa hawajaridhishwa kabisa na maamuzi ya JK, ukizingatia kwamba wamekuwa wakizunguka nchi kusisitiza kuwa watu wote walionufaika na fedha za ESCROW washitakiwe na wanyang'anywe mali zao. Pia rejea kauli za NKM wa CCM, Mwigulu Nchemba, wakati akiwa bungeni.
J. Mtatiro,
Jtatu, 22 Dec 2014,
Dar Es Salaam.



 Alicho Post
Eric Shigongo....

".......Hamjambo ndugu zangu, poleni sana shughuli za kujenga taifa? Bila shaka mmesikiliza hotuba ya Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete, mmeridhika? Kama hamkuridhika sana nina uhakika angalau nusu kidogo mmeona serikali yenu iko serious kila linapokuja suala la maslahi ya walio wengi.
Lakini nimejifunza kitu kimoja ..kumbe ni lazima kwanza kufungua mdomo na kuongea, hivyo basi tuachane na utamaduni wa kukaa kimya tunapoona mambo hayaendi vizuri. Hebu jiulize, vipi Kafulila asingekomaa? Vipi kama wabunge wa CCM waliokuwa ndani ya Kamati ya Zitto wangeamua tu kutetea maslahi ya serikali ya Chama chao? Waligoma kabisa, sababu ya maslahi ya walio wengi, kama kina mpina na FIlikunjombe waliamua kujitoa mhanga, wewe unaogopa nini kuwasha mshumaa wako kutokomeza uovu? AMKA SASA.
Umefika wakati wa vijana kuepuka uoga na kutete maslahi ya nchi! Badala ya kubaki tukisema tu, mnawona yule..alijaribu kupambana na sisitimu, mnamwona alivyo? Chezea system wewe! NAWAPONGEZA VIJANA WOTE WALIOJITOA MHANGA KUKEMEA UOVU HATA KAMA ULIWAGHARIMU MAISHA NA MALI, MUNGU ANAYAONA MACHOZI YAO, WATALIPWA KWA WAKATI MUAFAKA......." 


 Alicho Post
David Kafulila
From David Kafulila, Mb
1. Hoja kwamba pesa zilitolewa kwa uamuzi wa hukumu ya sept5.2013 sio sahh kwasababu hukumu ilisema ALL AFFAIRS OF IPTL SHOULD BE HANDED TO PAP. Haikusema kama escrow monies ni party of affairs of IPTL kwasababu zilikuwa kwenye mgororo. hoja ya kusema hukumu ilisema ilikuja baada ya kikao cha Oct8.2013 kunduchi beach hotel ambacho kiliongeza maneno kwenye hukumu kwa kusema ALL AFFAIRS OF IPTL INCLUDING RECEIBLES FROM ESCROW AC SHOULD BE HANDED TO PAP. Huko ni kupotosha hukumu kwani hela za escrow zilikuwa na mgogoro kati ya Tanesco na IPTL na PAP kununua IPTL haimanishi mgogoro kati ya IPTL na Tanesco umekwisha bali PAP ingechukua nafasi ya IPTL kwenye mgogoro wa pesa za escrow. hili Rais kapotoshwa.
2. Kusema Muhongo atamtoa bada ya uchunguzi wake ikulu kukamilika ni mbinu ya kumlinda kwani mbona mawaziri wanne waliohusika ktk oparesheni tokomeza ripoti ya bunge ilitosha rais kutengua uteuzi wao na kisha rais akaunda tume ya rais uchunguzi. kwann kwa Muhongo inakuwa kinyume chake?
3. Bunge liliazimia mamlaka ya uteuzi ichukue hatua dhidi ya Maswi. Rais anasema suala la Maswi ameliacha kwa mamlaka ya nidhamu ambayo ni Katibu Mkuu Kiongozi, Hapa Rais amekwepa Jukumu lake kwani yy ndio anateua na kufukuza Makatibu wakuu. pia suala hili sio jipya kwa Katibu Mkuu Kiongozi ingetosha awe amekwisha kuchukua hatua za kinidhamu siku nyingi kama TRA walivofanya kwa wahusika tawi la Ilala.
4. Hoja kwamba kutaifisha mitambo ya IPTL kutakimbiza wawekezaji ina mapungufu kwasababu kwa mujibu wa ripoti ya CAG, PAP alifanya utapeli wa kughushi katika umiliki wa IPTL hivyo sio mwekezaji mwadilifu hivyo kutaifisha haiwezi kutisha wawekezaji. pia ifahamike kwamba wawekezaji wengi wanatoka Ulaya na Amerika na nchi hizo ndio zimezuia misaada kutaka serikali itekeleze mazimio ya Bunge na mazimio ya Bunge ni pamoja na kutaifisha mitambo hiyo. sasa inawezekanaje nchi hizo zinazotaka serikali itekeleze mazimio kwamba ndio zikimbie kuwekeza kwa sisi kutekeleza mazimio husika? hapa ni namna ya kulinda matapeli wanaokuja kwa jina la wawekezaji
5.Hoja kwamba mikataba ikiwa wazi itakimbiza wawekezaji ina mapungufu kwasababu tatu;
a. Nchi nyingi sasa duniani mikataba ipo wazi na mfano rahisi ni Ghana na bado wawekezaji hawajakimbikia kwasababu hiyo. Ndio utekelezaji halisi wa itifaki ya OPEN GOVERNANCE ambayo Tanzania tulisaini

b. Kipengele cha Usiri(Confidentiality clause) kwa mikataba yote kinasema mkataba utakuwa siri isipokuwa kwa pande za mkataba(parties of contract) na kwa mahitaji ya dola( statutory purpose). sasa statutory purpose maana yake ni mahitaji ya Serikali, Bunge na Mahakama. sasa tatizo la sasa ni pale serikali inapokataa kutoa mikataba kwa bunge kwa hoja ya kipenge cha usiri(confidentiality clause) wakati kipengele hicho kinaruhusu Bunge kuwa na mamlaka ya kuona mikataba kama part of state organ
c. Pia wawekezaji hawa wanaposaini mikataba hapa wanakwenda kutafuta mitaji kwenye masoko ya mitaji kwao(stock markets). Kule kwenye masoko ya mitaji wanaweka wanalazimika kuweka mikataba hiyo wazi na wanaweka. hivyo kwa dunia ya leo ni aibu kuendelea kufanya mikataba kuwa siri.
6. Hoja ya kodi. TRA walidai kodi kwa barua kwenda BOT. na Werema ndio aliandika barua kukataa kodi. Kwakuwa CAG alikiri ktk ripoti kuwa kodi ilipaswa kulipwa kiasi cha 23bn mana yake alosema kodi isilipwe anapaswa kuchukuliwa hatua za kutaka kusababisha hasara hiyo. ikumbukwe Basil Mramba yupo mahakamani mpaka sasa kwa kesi ya kusababisha hasara ya 11bb. inawezekanaje hawa waishie kujiuzulu?
7. Mwisho kauli ya Mhe Rais kuwa fedha zile ni za IPTL kwasababu tu ziliwekwa kwenye escrow na Tanesco badala ya kulipwa moja kwa moja kwa IPTL kutokana na mgogoro sio sahh kwasababu pesa ya mgogoro kati ya Tanesco na IPTL haiwezi kuwa ya IPTL mpaka mgogoro umalizike na mwenyewe amekiri kuwa mpaka pesa hizo zinatolewa mgogoro ulikuwa haujamalizika. ni kwa mantiki hiyo pesa hiyo haikuwa sahh kuita ya IPTL. pia hapa niongeze kwamba Mgogoro wa IPTL kutoza zaidi Tanesco capacity charge unamanisha ni dhuluma ya IPTL tangu mwanzo wa utekelezaji wa mkataba mwaka 2002 na sio 2006 kama Mhe Rais alivosema. Hii ni kwasababu mgogoro wa IPTL ku overcharge Tanesco kwenye capacity charge msingi wake ni udanganyifu wa IPTL ktk mtaji na hivyo hesabu yake inapaswa kuzingatia tangu mwanzo wa utekelezaji wa mkataba mwaka 2002 na sio 2006 escrow ilipofunguliwa. Hii inakaziwa na Uamuzi wa mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara ( International Centre For Setllement Of Investment Disputes-ISCID) wa Feb12. 2014.
David Kafulila(MB)





Alicho Post
R.O.M.A

 ......and finally she z the WINNER!!! Huh?
hii ndiyo TANZANIA...
Wanaiba mamilioni hawachomwi wala hawafungwi/
Mtoto wa anko nyundo 2 jela kwa kuvuta bhangi/

Sasa niimbe nini tena ikiwa haya nilishayaimba MIAKA saba iliiyopita!!
Namuimbia MUNGU tu sasa MWANAKONDOO!!!




 Alicho Kipost
EDDO KUMWEMBE......
....Thanks for the memories Mama.. Nitakimiss kiburi chako.. Nakwambia haya in good faith.
Mdau wetu Naye;
Ame sema
Elasto Mbella

....Naona Mshua naye amekosa shabaha....
Anachengesha chengesha Wakati mimi Ninge lenga!
Sijui nayeye haja ona alenge wapi?????

Alicho Post
WANATUJUA VEMA, WALA HATUWEZI KUWAFANYA LOOTE BAYA KWAO:
Ndiyo, Mbwa ukimjua jina wala hupati tabu naye hata akibweka, akishupalia kubweka, unachofanya ni kumwita jina tu naye anatulia, ndicho kinachofanyika hata kwa utawala wan chi hii na watawaliwa,
Kwa yanachoendela nchini hapa, licha ya Rais Kikwete mwenyewe kujichanganya (Contradiction) katika hotuba yake, lakini nilichojifunza kwenye hotuba yake ile ni kwamba anajua fika kuwa Hata iweje hakuna kitakachofanyika hata akikengeuka juu ya maazimio ya Bunge,
Nikimnukuu Professor Kitila Mkumbo Anasema, “Watu watamshangaa Rais kama hatochukua maamuzi/ Hatua stahiki kwa MUHONGO, ni kama ameibua Hasira Zaidi kwa Watanzania,” Pia kasema “Rais ni kama anajicontradict na maelezo yake, kuhusu Pesa ni za Serikali au Wananchi, Maelezo yake yalikuwa yanajicontradict, ni kama alikuwa anajutia kwamba walifanya kosa”
Lakini nilichojifunza baada ya kufuatilia nyendo za Watanzania na Utawala wetu, niseme tu kuwa kinachofanywa na Serikali na kuhitimishwa na Kikwete leo, tunastahili kukipata. Yeah, wanatujua vema kuwa hatuwezi kufanya maamuzi yoyote dhidi yao, ndiyo maana yule mtoto mpendwa alisema pale Bungeni kuwa “Muhongo na Maswi, hawawezi kung’oka”
Nawauliza ninyi wabongo je mnapendezwa na kinachoendelea nchi? Mnangoja nini basi? Hivi na hili mnataka Mungu asiyeonekana ashuke kuwaambia kuwa kuna wizi unaofanywa na hizi Familia? Ndo maana nikasema Viongozi wanatujua vema kuwa Watanzania tu wapuuzi wa mambo yanayotuhusu, wacha wapete:
Lakini zaidi yayote Kwanini Werema Amejihuzulu, anawajibika kwalipi ikiwa zile pesa za Wananchi? Je Kwanini Tibaijuka Awajibike "Maadili" kwenye pesa zisizo za umma? Hahahahahahahaha, ngoja aondoke madarakani tutayajua mengi lakini kwanini umuwajibishe Tibaijuka kabla ya Muhongo? Hakika Muhongo amebeba SIRI ya Nishati na madini



TUNA SHUKURU KWA KUTUTEMBELEA!

Nukuu Zote zime kusanywa hapa MJUMBE BLOG

Kwa Ushirikiano wa Timu nnzima ya MJUMBE BLOG Mtandaoni ili kuwa rahisishia kazi wasomaji yetu kujua mitazamo ya baadhi ya watu ambao kwa namna moja ama nyingine ni Taswira ya jamii ndani ya Taifa letu.


Endelea kututembelea hapa MJUMBE BLOG kila mara ili ujipatie Picha,Matangazo,Habari,Taarifa kila siku.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top