Unknown Unknown Author
Title: UHALIFU:AJILIPUA AKI WALENGA POLISI!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Marehemu aliyetaka kuwalipua askari polisi kwa bomu Mtu mmoja (pichani juu) ambaye hajatambulika jina lake na anakotoka amefariki dunia ba...
Marehemu aliyetaka kuwalipua askari polisi kwa bomu Mtu mmoja (pichani juu) ambaye hajatambulika jina lake na anakotoka amefariki dunia baada ya kulipukiwa na bomu huku utumbo wake ukiwa nje na mkono wake kukatika alilotaka kuwarushia askari polisi waliokuwa doria usiku wa kuamkia leo na kujeruhi askari polisi wawili ambao hali zao zinaendelea vizuri. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu ameiambia ITV kwa njia ya simu kuwa watu wanne waliokuwa na mtu huyo walikimbia huku polisi wakikamata simu za watu hao pamoja na ya marehemu huyo na kwamba hili ni tukio la tatu la mabomu dhidi ya askari Polisi. Amesema kukamatwa kwa simu hizo ni mwanzo mzuri wa kuwabaini walipuaji mabomu kwa askari polisi mjini Songea. Mkuu huyo amesema kuwa kutokana na uzito wa tukio hilo, Mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini CP Isaya Mungulu anafanya safari ya Songea leo na atazungumza na vyombo vya habari. Mwandishi wa habari hii aliyekuwepo eneo la tukio alishuhudia mabaki ya bomu hilo pamoja na mzula wa kuziba sura aliokuwa akiutumia mtu huyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top