UKATILI:PICHA APIGWA! ATESWA NA KUTELEKEZWA AFIE MBALI!
Pichani ni wasamalia wema Wakiustiri mwili wa Kijana ambaye jina lake kamili haliku patikana mara moja baada ya kufariki katika mazingira ya kutatanisha
Sehemu ya umati ulio jitokeza kushuhudia tukio hilo la kustukiza na lililo zua sintofahamu kwa wakazi wa Kibororoni,Moshi
Picha zaidi ziionesha baadhi ya Mashuhuda hapo juu
Majira ya Mchana Mida ya saa Saba na robo,Mitaa ya Kibororoni;Mjini Moshi!
Nitukio lililo zua taharuki Katika mtaa wa Kibororoni,Mjini Moshi Kilimanjaro pale ambapo kijana aliye fahamika kwa Jina Moja tu la MANJO alipo kutwa katika kolongo lilipo eneo la Mtaa wa Kibororoni,Mjini Moshi huku akitoa povu na Damu kinywani mwake.
Akiwa anaomba msaada kwa wasamalia wema wampe maji ya kunywa na mara baada tu ya kupewa maji alikata kauli na kufariki.
Baadhi ya mashuhuda walio kuwepo eneo la tukio walimwelezea marehemu kama kondakta wa moja ya daladala za mjini Moshi,Na wali zidi kueleza kuwa muda mchache ulio pita walikutana naye akiwa mzima;Lakini baada ya muda kidogo tu wali pigiwa simu na kuelezwa kuwa ndugu yao huyo alikuwa akipigwa na wananchi wenye hasira kali walio mtuhumu kuwaibia.
Wakati ndugu zake hao wa karibu wakiwa katika harakati za kumtafuta ndipo walipo Mkuta MANJO Akiwa hajitambui kolongoni.Mpaka Mpiga picha wetu anaondoka eneo la tukio hakuna mtuhumiwa aliye husishwa na tukio hilo la mauaji aliye fahamika,Kwani wauaji hao baada ya kutekeleza unyanyasaji wao huo na ukatili wali mtelekeza na kumwacha,Kipigo ambacho kilipelekea umauti wake.
Ambapo baada ya muda mfupi polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu ili kwenda kuuhifadhi.
Picha na Maelezo
Mdau wa MJUMBE BLOG
Kilimanjaro
Moshi
Tuna shukuru kwa kututembelea.
Shukrani.




Post a Comment