Pichani ni kituo kinacho itwa Nsenjere ya Pili unapo tokea Mbeya Kuelekea Tunduma,Hapa mida ya Mchana huwa wana simama Wazee wa Tochi ili kuhakikisha Usalama Barabarani.
Ni Jioni ya siku ya Alhamis,Kamera yetu ya MJUMBE BLOG ime amua kuya angazia maeneo ya Nsenjere,Wilayani Mbozi Mbeya,Pichani ni wanafunzi wa shule ya msingi wakirudi majumbani kwao
Pichani ni Miongoni mwa shughuli z kiuchumi ambazo wanazifanya wakazi wa Nsenjere,Mbozi eneo ambalo lina aminika kuwa hatari zaidi kwa abiria na madereva nyakati za usiku
Hapa nipo Mita Miatano Kutoka kilipo kituo cha Nsenjere Uelekeo wa Stend ya IYULA,Kimvua kina nyesha kwa mbali Magari mengi yana pita kwa kasi na hakuna Dereva wala abiria anaye weza akathubutu kukuamini hata kama ukisimamisha gari yake! Kwa Hapa Wana amua kukinai abiria kwa muda kwanza huku wakkiomba wapite pori hili salama! Sehemu ambayo imekuwa ikiaminika ni hatari kwani kuna Uporaji wa mali kwenye magari hufanyika mara kwa mara.
Naam,Ukifika Nsenjere utakutana na Maandishi haya upande wa Kushoto Mita kama mia saba kutoka ilipo stendi ya Nsenjere au Mita kama Mia nne Kutoka ilipo Njia panda ya Iyula ni eneo ambalo Kama dereva akikuona ana Ongeza kukanyaga mafuta tu na kufunga vioo na kujihami zaidi
Pichani ni Kiini cha Eneo ambalo lina aminika ni hatari kwa Wasafiri wa Endao Wilayani Mbozi,Eneo hili Ina aminika na wenyeji wa Mbozi au Madereva kuwa hatari Usiku Kuliko Ndege itakapo feli injini ikiwa angani na abiria ndani yake! Kupita hata salama ni Kudra za MUNGU tu na haitakiwi uwekee mazoea kwani utakuwa una Hatarisha Maisha yako kwa Makusudi kabisa.
_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
Nime Jaribu kusimamisha magari eneo hili lakini hakuna aliye jaribu kusimama,Na hao walio simama hapo juu pichani hawana jinsi kwani Magari yao yame haribikia eneo husika! Nime abiri kwenye Pikipiki ya Jamaa ambaye baada ya kumsimamisha alisimama mita chache mbele huku akiwa ame jihami na kukubali kunipa lift! Hapo alinambia laiti kama isinge kuwa Mavazi yako Uliyo vaa kuwa yenye Mwonekano Nadhifu na haiba yako,Nisinge Simama hapa! Na hapa ana zungumuzia UZI WANGU HUU WA TAIFA Wenye maneno TANZANIA Kifuani! Dereva wangu huyu anakiri kuwa Hili ni eneo Hatari kwa wasafiri kwani kuna vijana ambao hudandia magari nyakati za usiku na Kushusha Mizigo mbalimbali ambapo vijana wengi wame poteza maisha kwani kuna madereva ambao huwa wame jihami kwa namna moja ama nyingine!
_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
Picha Zote Na MJUMBE MTAZAMAJI,Mbeya,Mbozi
Post a Comment