Sehemu ya Umati Ulio jitokeza katika ziara ya Mheshimiwa SUGU kama anavyo julikana na wengi katika mji wa Vwawa leo jioni
Kiongozi mwandamizi wa wilaya ya Mbozi akijigamba kutimiza ahadi ya kutwaa mitaa mingi katika makao makuu ya wilaya kama alivyo wa ahidi wananchi kabla ya Uchaguzi
Mwalimu Pascal Haonga akijaribu kutoa neno la shukrani kwa baadhi ya wanachi walio jitokeza katika ziara ya Mhe.Joseph Mbilinyi baada ya kupewa fursa hiyo
Pichani ni Katibu(chini) na Mwenyekiti wa BAWACHA mkoa wa Mbeya waki wasalimu baadhi ya wananchi wa Vwawa walio jitokeza katika makutano hayo katika mji wa Vwawa leo jioni,
Pichani juu ni Shombe Fadhiri aliye jitambulisha kama Mwanasheria wa CHADEMA Nyanda za juu kusini akitoa nasaha kwa wapiga kura watarajiwa wa Mji mdogo wa Vwawa,Mbozi jioni leo
Pichani juu ni Mkisi ambaye alijitambulisha kama moja kati ya wanajopo wanao fanya Utafiti wa Sera za Chama Nyanda za Juu Kusini akitoa Sera zake kwa Wananchi wa Mji Mdogo wa Vwawa jioni ya Leo
Pichani ni Mheshimiwa diwani wa Kata ya Mlowo Ndugu Mwang'amba akitoa Nasaha katika mji mdogo wa Vwawa leo jioni na kutoa Shukrani kwa wananchi na wakazi wa Vwawa kwa kuwapa imani ili CHADEMA iwaongoze kwa kipindi kijacho.
Moja ya Viongozi waandamizi wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya aliye Jitambulisha kama MBU MWENYE UWEZO WA KUSAMBAZA MALARIA kwenye majimbo ya chama tawala,Picha ya chini aliwaomba wana nchi wa Vwawa,Mbozi wanyoshe Mkono wao juu kwa Muda wa dakika moja tu kama ishara ya kuwa kumbuka baadhi ya wananchi na wafuasi wa CHADEMA walio
uawa katika maeneo mbalimbali ya nchi;Kwa kuwataja majina yao,GEORGE NGUGULI ambaye naye alipigwa risasi Arusha na polisi,MSAFIRI MBWAMBO mwenyekiti wa CHADEMA aliye chinjwa na watu walio dhaniwa kuwa wafuasi wa Chama tawala,ARIZONA muuza magazeti aliye uawa kwa kupigwa risasi mjini morogoro,DAUDI MWANGOSI,aliye uawa kwa kupigwa risasi na polisi pia,eneo la Nyororo!
Mama mwenye baiskeli ya kusukumwa kwa mikono naye akiwa eneo la Umati ulio jitokeza kusiliza neno la shukrani kutoka kwa CHADEMA leo jioni katika Mji wa Vwawa
Waongoza Msafara wa Mheshimiwa Sugu waki wasiri katika eneo la tukio katika mji wa Vwawa,Mbozi leo jio ndani ya mavazi yao rasmi kama wanavyo onekana pichani
Mheshimiwa SUGU ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi akiwasiri eneo la tukio katika mji wa Vwawa,Mbozi
Mhe.Sugu akiwa amesha chukua nafasi yake huku akiteta jambo na watangulizi wake eneo la tukio
Sehemu ya Viongozi waandamizi wa CHADEMA walio kuwepo eneo la tukio meza kuu
Chifu Msanganzila,ambaye alijitambulisha kama katibu wa machifu wilaya akihutubi umati ulio hudhuria kwa kusisitiza Amani na Utulivu huku akisisitiza kwamba tuna weza kutofautiana misimamo kwa kugombanisha hoja zetu na kuwa achia wananchi ambao ni kama wateja wa Vyama vyote wachague bidhaa yao kwa kutazama Mzani ambao una watendea haki! Yeye alijitambulisha kama alama ya AMANI NA UTULIVU katika makutano walio kuwepo Vwawa jioni ya leo

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi SUGU akiwa jukwaani kwa ajili ya kutoa ufafanuzi zaidi kwa wananchi na wakazi wa Vwawa leo jioni;Ame zungumzia zaidi suala la Kubunguliwa kwa mahindi ya wakulima wengi katika maghara ya taifa bila wao wenyewe kulipwa fedha ile hali pembejeo ziko juu,Pia ali wasisitiza wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu mara serikari itakapo tangaza kuanza kwa Zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya daftari la kudumu la kupigia kura,Pia Aligusia suala la Katiba mpya na kusisitiza kuwa katiba inayo pigiwa debe na CCM ime chakachuliwa na ni mbovu kuliko hata ile ya zamani! Ali waomba wananchi wa ikatae na kusema kuwa Akina Mzee Warioba na Mzee Kaduma wanamjua mwalimu Julius Nyerere Kuliko hao wanao pita majukwaani kuinadi katiba husika inayo pingwa na hao wazee.
Baadhi ya wanachama walio kuwa wa Chama tawala waki mkabidhi kadi zao Mhe.Joseph Mbilinyi na Kukabidhiwa kadi mpya za CHADEMA mbele ya umati ulio jitokeza
Pichani juu ni Taswira ya sehemu ya Umati ulio jitokeza kwenye ziara ya Mhe.Sugu Wilayani Mbozi,Vwawa jioni ya leo
_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
Shukrani ya Picha zote NA MJUMBE MTAZAMAJI,Aliye kuwepo eneo la tukio
Post a Comment