Unknown Unknown Author
Title: DULLY SYKES ASUSIWA MSIBA NA WASANII WENZAKE! DIAMOND ATAJWA,KUCHAGUA MISIBA!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
IMEKULA kwake! Wasanii wa sinema na Bongo Fleva wamemchana vibaya staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul 'Diamond' kwamba si ...

IMEKULA kwake! Wasanii wa sinema na Bongo Fleva wamemchana vibaya staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul 'Diamond' kwamba si mtokaji kwenye misiba ya wenzake.
Wakizungumza na Amani kwenye maziko ya baba mzazi wa Mbongo Fleva, Abdul Sykes 'Dully Sykes', Ebby Sykes, Jumatatu iliyopita, wasanii hao walioomba majina yao yalindwe walisema kumbukumbu za vichwani mwao zinaonesha kuwa, Diamond amekuwa akichagua misiba ya kujitokeza hasa ile ambayo itampa 'kavareji' kwenye vyombo vya habari.

WASIKIE WENYEWE
"Mimi nakumbuka wakati wa kifo cha Kanumba (Steven), Diamond alitokea kwa sababu ulikuwa msiba mkubwa sana na kweli alipata kavareji ya kutosha kwenye media.

"Halafu akaonekana tena kwenye msiba wa baba yake Wema Sepetu, nadhani kwa vile alikuwa mtu wake Wema wakati huo asingeacha kwenda. Lakini baada ya hapo sikumbuki," alisema msanii mmoja.
Msanii mwingine aliongeza: "Halafu Diamond na Dully ni washikaji, sasa jamaa tunasikia yuko Zenji tu hapo anakula bata na Zari (Zarina Hassan) lakini ameshindwa kuja Dar kumzika baba mzazi wa mshikaji wake."



BAADA YA WA WASANII WENGI KUTOHUDHURIA MAZISHI YA BABA YAKE DULLY SYKES!
MWENYEWE AMESEMA HAYA:


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes, ameshangazwa na kitendo cha wasanii wengi kutojitokeza katika mazishi ya baba yake mzazi, Ebby Sykes juzi jijini Dar es Salaam.



Akizungumza jijini juzi mara baada ya kumalizika kwa mazishi ya baba yake, msanii huyo alisema ameshangaa jinsi gani wasanii wengi wamekuwa na roho za chuki.

Alisema matarajio yake yalikuwa kuwaona wenzake wakiungana naye katika wakati huo mgumu, lakini ni wachache sana walioonyesha moyo wa upendo na ukaribu.


"Nilitegemea kwakuwa tunampumzisha baba yangu hapa hapa Dar es Salaam, wangekuja wasanii wengi ambao ni marafiki zangu, lakini hali ilikuwa tofauti kabisa," alisema.



MJUMBE BLOG
Tuna kupongeza kwa kuamua kutumia huduma zetu.
Karibe tena.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top