Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kujitokeza kupatiwa msaada wa kisheria, na wasaidizi wa kisheria waliopo wilayani hapo ili kuwasaidia kutatua migogoro mbalimbali inayowakumba kutokana na ukosefu wa elimu ya sheria.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama cha wasaidizi wa kisheria wilayani Makete PACEMA ambaye pia ni msaidizi wa kisheria kata ya Lupila Bw. Nebert Sigala wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusu elimu ya masuala ya kisheria katika kata hiyo.
Bw. Sigala amesema kwa hivi sasa wapo wananchi ambao wamekuwa wakijitokeza kupatiwa msaada wa kisheria ambao umekuwa ukiwasaidia katika matatizo yaliyokuwa yakiwakabili kwa kuwa hawakuwa na uelewa huo toka awali .
Ametaja baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa yakihitajika zaidi na wananchi hao kuwa ni sheria za ardhi, sheria ya mtoto pamoja na sheria mbalimbali za nchi, jambo ambalo limewasaidia wananchi wa kata hiyo kuona umuhimu wa kumiliki ardhi kisheria.
Credit:Maiko Luoga
MJUMBE BLOG
Tunashukuru ndugu mtembeleaji wetu kwa kutupa fursa tukuhudumie
Post a Comment