Unknown Unknown Author
Title: PICHA ZINA HUZUNISHA:MWANA WA NCHI ANA LENGWA NA CHOZI LA UPWEKE!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Nchi ni watu.Uhai wa nchi ni Uhai wa watu.Afya ya watu ndio afya nchi. Rasilimali watu ndio msingi muhimu wa maendeleo kwa taifa liwalo lo...
Nchi ni watu.Uhai wa nchi ni Uhai wa watu.Afya ya watu ndio afya nchi.

Rasilimali watu ndio msingi muhimu wa maendeleo kwa taifa liwalo lote lile duniani.
Hili lina weza kujidhihirisha kwa mifano ambapo kuna mataifa hayana hata aridhi isiyo kaliwa Lakini yamekuwa ndiyo mataifa ya kwanza kutoa misaada kwa mataifa yenye utajiri wa aridhi na Rasilimali zingine.
WENZETU HAWA WAME WEKEZA KWENYE WATU;NA SIO KWENYE VITU!!
Endelea kufuatilia uzi huu:




Pichani ni mtoto ambaye jina lake haliku fahamika mara moja akiwa amelala usingizi mzito chini ya mti kando ya makutano ya njia pacha katika moja ya kijiji nchini.


Mtoto huyo aki amshwa na Mdau wa MJUMBE BLOG kijijini ili kumwondoa njiani hapo na kumpeleka mahali salama zaidi.


[17:01, 2/21/2015] Elasto Ngaya: Ni alasiri moja tulivu;
Mtembea bure anakatiza mitaa ya kijijini hapo.Kando ya njia hiyo ana mwona mtoto 'aliye kalala' kama anavyo onekana pichani.

Ana mwamsha kisha ana mnyoshea mkono ishara ya kumnyenyua!

Mtoto naye ananyenyua mkono wake(huku ana gumia kwa kulia na akitokwa machozi) na kuufungamanisha na na ule wa MTEMBEA BURE!

Akiwa ame simama;anaAnalysis ulizwa Nyumbani wapi? Ana elekeza kwa mkono wake kuwa palee....

Mita kama mia mbili hamsini hivi;kutoka pale alipo kuwa ame lala.Unakutana na wigo na mlango unao ingia panapo sadikika ni nyumbani kwa mtoto huyo.

Mlango wa nyumba ume fungwa! Hodi ina pigwa hakuna mwenyeji anaye itukia,Ndani ya ua ule kuna kama kipande cha Mkeka na nguo kitenge ikiwa ime anikwa!

Mdau ana Chukua kipande kile cha mkeka na Kumtandikia yule Mtoto na kumwacha apumzike pale kivulini kwenye mti ulio kuwa pale ndani!

Ana ondoka akimwacha yule mtoto ana mchungulia kupitia pale alipo lazwa...


Naam;
Wahenga wana msemo kuwa KUZAA SIO KAZI;KAZI KULEA MWANA!!

Maisha ya Mwana wa nchi huyu yana thibitika kwa vitendo! Maisha ya kuishi kama digidigi..

Mzazi Una jua mwanao ame lala wapi? Anacheza wapi? Ame kula nini? Ame vaa nini?
au kuna ndugu une watelekezea Mzigo wa kulea?

Ume kwepa wajibu wako wa jukumu la kuitwa Mzazi! Unajiona bado mtoto.Una jitoto esha.

Kumbuka mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.Mtoto wako ni Taswira halisi ya Tanzania Tuitakayo! Ni tumaini la Tanzania ijayo.Udhaifu wa Malezi yako ni maandalizi ya kuwa na Taifa dhaifu.

TANZANIA kama taifa hatu hitaji kuwa na idadi ya watoto wengi walio kosa afya na malezi bora ya kimwili na Kiroho...
Tuna hitaji tuwe na idadi ya wastani kwa uzao kwenye kila familia;Lakini WATOTO WETU Lazima tuhakikishe wanakuwa wenye afya bora na wana pewa malezi ya msingi na wazazi husika! Na wala sio na akina bibi zao! au Wasaidizi wetu wa kazi jambo ambalo linasababisha watoto wetu wasifanane na vile tunavyo tamani wawe...
UKI ZAA WAJIBIKA! USI KWEPE MAJUKUMU.


Na tusi wafanye wana wa nchi kutoa machozi yatakayo Lowanisha udongo usio na hatia.
Picha na Maelezo yote:
Mdau wa MJUMBE BLOG,
Kutoka kijijini.




MJUMBE BLOG
Tunashukuru kwa kutupa fursa ya kukuhudumia.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top