Kutoa siri za taifa kubwa kama Marekani ni kesi kubwa sana, iwapo wakikukamata watu wa usalama wa nchi hiyo na ukafikishwa Mahamakani ni ishu kubwa ambayo hata Edward Snowden inamtia hofu.
Snowden alikuwa mmoja ya wafanyakazi wa CIA, baadaye aliendelea kazi sehemu nyingine ikiwemo Kampuni ya Dell kutokana na utaalamu wake kwenye masuala ya computer, jina lake liliingia kwenye headlines kubwa duniani baada ya kuvujisha taarifa za siri za ndani za taifa la Marekani, ikiwemo ishu ya watu wa usalama wa nchi hiyo kuchunguza simu mbalimbali pamoja na za viongozi wa mataifa mengine duniani.
Mwanasheria wa Edward Snowden amesema jamaa huyo yuko tayari kabisa kurudi Marekani lakini atarudi kama watamhakikishia haki kutendeka wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake.
Mwanasheria huyo Anatoly Kucherena amesema Snowden ana hamu kubwa kurudi nyumbani kwao Marekani lakini hofu yake kubwa ni jinsi ambavyo atapokelewa japo Mwanasheria Mkuu wa Marekani kamuahidi kwamba hatohukumiwa kifungo cha maisha.
Snowden bado anaweza kusafiri kwenda sehemu nyingine yoyote duniani kutokana na kwamba ana hati ya kuishi Russia kwa miaka 3 na amekuwa ndani ya nchi hiyo kwa kipindi chote ambacho amekuwa akitafutwa na Marekani baada ya kuvujisha siri hizo.
Wenzetu huwa hawakawizi mambo, unaambiwa huu utata wa maisha ya Snowden tayari wameingia location wanaandaa filamu ya maisha yake muda wowote ikitoka huenda tukamfahamu zaidi jamaa huyo kupitia movie hiyo ambayo actor Joseph Gordon-Levitt ndio star ambaye amecheza kama Snowden.
MJUMBE BLOG
Tupo mtandaoni kwa Picha,Matukio,Habari,Matangazo na Stori zinazo gonga vichwa vya habari.
Post a Comment