WAKATI wimbo wa ‘Hawajui’ wa msanii, Vanessa Hau Mdee ‘Vee Money’, ukiongoza katika chati za ubora za vituo mbalimbali vya redio na runinga za nchini Nigeria, msanii huyo amesema wasanii wengi hawajui namna ya kutumia mitandao ya kijamii kuuza kazi zao.
Vanessa alieleza hayo jana alipotembelea ofisi za Kampuni ya New Habari (2006) Ltd inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, Rai na The African, akiwa katika harakati za kutangaza wimbo wake mpya wa ‘No body but Me’ aliomshirikisha rapa mkongwe KO kutoka Afrika Kusini. Wimbo huo utaanza kusikika katika vituo vya redio na kuonekana katika runinga mbalimbali kuanzia siku ya Alhamisi.
Vanessa amekuwa mfano wa wasanii wanaonufaika na kazi zake kupitia mitandao mbalimbali, lakini wasanii wengi hawajui namna ya kunufaika nao ndiyo maana wanaonufaika na kazi hizo za mitandaoni si wasanii wenye kazi zao.
“Wasanii wengi hawajui namna ya kujiandikisha, hawatambui namna ya kuuza kazi zao kupitia mitandao lakini naamini wapo baadhi ya watu wananufaika na kazi za wasanii hao mitandaoni bila wao kujua,’’ alisema huku akiwataka wasanii waweke mazoea ya kujiandikisha katika mitandao hiyo ili wanufaike nayo
“Mimi nina watu zaidi ya 300,000 wanaofuatilia muziki wangu hivyo zipo kampuni kupitia nafasi hiyo mitandaoni zinafanyakazi nami kwa malipo mazuri, pia natumia kampuni hizo kutangaza kazi zao kupitia muziki wangu nao wananilipa hadi wakati mwingine fedha hizo natumia kwa ajili ya kuandaa video za nyimbo zangu,’’ alieleza Vanessa.
Post a Comment