Muimbaji maarufu wa Rwanda amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kushtakiwa kwa njama za kutaka kumuua Rais Kagame na kuonyesha chuki dhidi ya serikali.
Kizito Mihigo awali alisema alikuwa na makosa na kuomba msamaha, akimaanisha hukumu yake ipunguzwe.
Kizito Mihigo amekuhumiwa jela miaka 10 kwa njama za kutaka kumuua Rais Paul Kagame
Mshtakiwa mwenzake, Cassien Ntamuhanga kiongozi wa kituo cha redio ya Kikristo, alifungwa miaka 25 kwa ugaidi na matusi.
Ameendelea kukataa mashtaka yote.
Mihigo alikubali kutumiana ujumbe na kundi la upinzani lenye maskani Afrika Kusini, Rwanda National Congress (RNC).
Alifutiwa mashtaka ya ugaidi huku Ntamuhanga alifutiwa kosa la kupanga kumuua Rais Kagame.
MJUMBE BLOG
Tunashukuru kwa kutupa fursa tukuhudumie.
Karibu tena.
Post a Comment