Unknown Unknown Author
Title: PIGIENI KURA YA NDIO KATIBA MPYA -SALMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete amewaomba wananchi k...




MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete amewaomba wananchi kuipigia kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa, kwa kuwa ni bora na imezingatia mahitaji ya makundi yote ya jamii.

Mama Kikwete ambaye ni mke wa Rais, Jakaya Kikwete alitoa ombi hilo jana wakati akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara, uliofanyika katika tawi la Mikumbi Magharibi kata ya Wailes wilayani humo.

Alisema Katiba Inayopendekezwa ni ya watanzania wote na imegusa maeneo yote muhimu kwa ustawi wa wananchi, kama vile haki za wanawake, wazee, wavuvi, watoto na watu wenye mahitaji maalum.

Pia, aliwahimiza wananchi hao kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa na kushiriki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu wa kumchagua diwani, mbunge na Rais.

Alisisitiza, “Kazi hii ya uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura ni mpya, hata kama una kitambulisho cha zamani ni lazima ujiandikishe. ”

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza aliwataka wazazi na walezi kuona umuhimu wa kusimamia elimu ya watoto wao, kwani wakisoma wataweza kuzitumia fursa za kitaalam zinazopo mkoani humo.

Alisema hivi sasa shule za msingi na sekondari ziko nyingi, lakini cha kushangaza kuna baadhi ya wazazi hawataki kuwapeka watoto wao shule.

Katika mkutano huo, wanachama wapya 202 walijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo wawili kati ya hao walitoka Chama cha Wananchi (CUF)

.CHANZO:HABARI LEO

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top